VINCENT ARIEMBA AACHIWA KWA DHAMANA
Vincent Ariemba Moisabi ameachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu ya Ksh.30,000 au dhamana ya Ksh.50,000 na mdhamini wa kiwango sawa juu ya kosa linalodaiwa la shambulio.
Moisabi anadaiwa kumshambulia Chifu Msaidizi Zebedeo Onditi mnamo Mei 4, 2021 katika eneo bunge la Bonchari.
Mtuhumiwa huyo - ambaye aliwakilishwa na mawakili Edward Begi, Wilkins Ochoki na Kerosi Ondieki - walikana mashtaka mbele ya Hakimu Mkuu Nathan Shiundu.
Wakili kiongozi Edward Begi alisema kuwa mjumbe wa Bunge la Kaunti ya Kisii ni mtu maarufu kwa hivyo anapaswa kupewa dhamana ili aendelee kuhudumia umma.
Kesi hiyo itatajwa mnamo Mei 13, 2021.
Post a Comment