TUPANDE MITI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.. Selemani amesema ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi tunahitaji kupanda miti kwa wingi katika maeneo mbalimbali nchini.

Jafo amesema hayo Jana Mei 29 wakati wa zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Medeli jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.

Aliwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda maeneo ya nchi yetu yasiendeele kugeuka kuwa jangwa na kuwa ili kukabiliana na hali hiyo Ofisi ya Makamu wa Rais imekuja na Kampeni kabambe ya Usafi wa Mazingira na Utunzaji wa Mazingira.

Aliongeza kuwa kampeni hiyo itasaidia katika kuondosha hali hiyo kwa kumshirikisha kila mtu kwa nafasi yake aweze kuwa sehemu ya kuhifadhi na kutunza mazingira.

Aidha, Waziri Jafo alisema kuwa Halmshauri zote nchini zinapaswa kupanda miti isiyopungua milioni 1.5 kila mwaka ili kukabiliana na chanhamoto ya mabadiliko ya tabianchi.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka alisema uongozi wa mkoa huo uko utapokea na uko tayari kutekeleza maelekezo yatakayotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Selemani Jafo ameshiriki matembezi ya hiari ya upandaji miti ikiwa na lengo la kukiijanisha Dodoma kuelekea siku ya Mazingira Duniani huku akizitaka Halmshauri zote hapa nchini kupanda miti isiyopungua Milioni moja na laki tano kila mwaka .

Matembezi hayo yamefanyika leo Mei 29,2021 jijini Dodoma yaliyoanzia  viwanja vya Bunge kuelekea eneo la Medeli ambapo shughuli ya upandaji miti imefanyika na kuhudhuriwa 

 “Hii ni siku maalumu kwa ajili ya upandaji wa miti,nawashukuru waliokubali wito wa kukubali kuja katika siku hii ya upandaji miti.

No comments