RAIS SAMIA ATOA MAAGIZO KWA MAAFISA HABARI

Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa
salamu na maelekezo mahususi kwa Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki kwenye
ufunguzi wa kikao kazi cha 16 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano (TAGCO) Jijini
Mbeya.

Amesema "Muendelee kuhimizana umuhimu wa taarifa za kazi zenu kwa umma, yale mazuri au
hata yasiyoridhisha lazima kuwe na namna ya kutoa taarifa kwa umma. Msiache mpaka wananchi wanaolalamika na kudai kuelezwa lililopo ndio taarifa inatolewa. Vinginevyo nawatakia mkutanobmwema na kazi iendelee".

Ni ukweli usiopingika kuwa katika zama za sasa endapo taaluma ya habari ikitumika kimkakati
itasaidia kutimiza malengo ya Serikali.

Tunafurahi kuona kuwa katika kuhitimisha kikao hiki wanachama walijadili namna bora ya kute-
keleza maelekezo hayo ya Mhe. Rais na hotuba ya Waziri Bashungwa chini ya uenyekiti wa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari Dkt. Hassan Abbasi na kuahidi kuyafanyia kazi kikamilifu. 

Tunachukua nafasi hii kumshukuru na kumpongeza Mhe. Rais kwa kutambua mchango wa Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki serikalini katika kuelezea shughuli mbalimbali za Serikali.

Tunaamimi maelekezo haya ni chachu na mwanzo mpya wa ufanisi wa kazi kwa Maafisa Habari
katika kuisemea Serikali.

Sisi Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tunaona kauli ya Mhe. Rais imeitoka katikanwakati mwafaka ambapo Serikali inafanya mambo mengi yanayopaswa kupelekwa kwa wananchibili wafahamu, waiamini, waikubali na washiriki kikamilifu katika kutekeleza hatimaye kujenga uchumi imara wa nchi yetu.

Tunapongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Wizara chini ya Mhe. Waziri Innocent Lugha
Bashungwa (Mb), Naibu wake Pauline Gekul (Mb) na Menejimenti ya Wizara ikiongozwa na Katibu
Mkuu Dkt. Hassan Abbasi na Naibu wake Dkt. Ally Possi kwa kutoa miongozo na usimamizi thabiti
wa Sera na maelekezo mbalimbali ya viongozi Wakuu wa nchi.

Kwa upande mwingine tunatoa pongezi za dhati kwa Katibu Mkuu wa Wizara yetu Dkt. Hassan
Abbasi kwa tunukiwa tuzo ya pongezi na TAGCO kwa mchango na mageuzi makubwa aliyoyaleta
katika kipindi chake akiwa kwenye nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO na
Msemaji wa Serikali.

Tunaungana na kauli ya Mhe. Rais, maelekezo yake pamoja na salamu inayosisitiza kuiheshimu na kuipenda nchi yetu kwa kusema "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kazi lendelee."

No comments