RAIS SAMIA AONYA VITENDO VYA UJAMBAZI DSM
Rais Samia Suluh Hassan ameonya vitendo vya ujambazi vilivyoibuka Jijini Dar es Salaam na kusema wasipime kina cha maji na wasimjaribu.
Rais Samia ameyasema hayo wakati akizungumza na wazee wa jiji hilo jana katika ukumbi wa mikutano wa Mliman City na kusisitiza kuwa vitendo hivyo hatavivumilia hivyo ni vyema wanaojihusisha na ujambazi watafute kazi za kufanya.
"Hivi karibuni kumeibuka upya vitendo vya ujambazi jijini Dar es Salaam, nimeona kwenye mitandao watu wanasema sema na kulalamika hadi kufikia kuomba arejeshwe kamanda fulani, nawaonya wasipime kina cha maji na wasijaribu hata kidogo,"alisema.
Alimtaka IGP Simon Sirro, kufanyia kazi tuhuma hizo na wazee kuzungumza na watoto wao kwakuwa hata kama kuna hali ngumu ya uchumi haisababishi watu kujihusisha na vitendo vya ujambazi.

Post a Comment