RAIS SAMIA AMEMSIMAMISHA KAZI DC SABAYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Bw. Lengai Ole Sabasa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Bw. Sabaya amesimamishwa kazi kuanzia leo tarehe 13 Mei, 2021.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Samia amemteua Bw. Nsubili Akomeligre Kajela Joshua kuwa Karani wa Baraza la Mawaziri. Ber. Joshua alikuwa akikaimons nafasi hiyo.

Mhe. Rais Samia amemteua Bw. Ayub Musa Makoye kuwa Naibu Karani wa Baraza la Mawaziri. Bw. Makoye alikuwa akikaimu mafasi hiyo.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Samia amemteua Dkt. Stergomena Tax kuwa Mwenyekiti
wa Bodi ya Taasisi ya Uongozi (longuzi Institute). Dkt. Tax ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Mhe. Rais Samia amemteua Dkt. Laurian Ndumbaro kuwa Makamu Mwenyekiti wa Taasisi
ya Uongozi. Dkt. Ndumbaro ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Sambamba na uteuzi huo, Mhe. Rais Samia amefanya uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Taasisi
ya Uongozi ambao ni Balozi Riitta Swan, Prof. Penina Mama, Bi. Lina Sori, Bw. David Walker, Bi. Suzan Mlani, Dkt. Hamis Mwinyimvua na Prof. Samwel Wangwe.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 13 Mei, 2021. 

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Samia amemteua Bw. Ishmael Andulile Kasekwa kuwa
Mwenwekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADIA.

Uteuzi wa Bw. Kasekwa umeanza tarehe 10 Mei, 2021 na amechukua nafasi ya Dkt. Rosebud
V. Kuwa ambaye amemaliza muda wake.

No comments