NDALICHAKO AKIPONGEZA CHUO CHA KILIMO CHA SUA

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa jitihada wanazozifanya katika kuibua Wabunifu,Teknolojia na mbinu zingine za kisayansi pamoja na kuwa saidia na kuendeleza wabunifu hao ili waweze kufikia ndoto zao na kusaidia jamii na taifa.

Pongezi hizo ametoa wakati akitembelea kukagua kazi za wabunifu wa SUA na maonesho yao kabla ya kuzindua rasmi mashindano ya kitaifa ya sayansi,teknolojia na ubunifu (MAKISATU 2021) jijini Dodoma yanayokutanisha wabunifu kutoka nchi nzima kwenye makundi saba ya ushindani.

Akizungumza wakati akifungua mashindano hayo amesema kuwa miongoni mwa mafanikio ambayo Serikali imeyapata katika kuendeleza Sayansi na Ubunifu nchini ni pamoja na kuibua na kutambua wabunifu wachanga 1066 kupitia MAKISATU 2019/2020 ambapo kati ya hao wabunifu mahiri 130 wanaendelezwa na Serikali ili bunifu zao zifikie hatua ya kubihasharishwa na hivyo kuongeza fursa za ajira kwa vijana na kuchangia kwenye pato la taifa.

No comments