MKUTANO WA BARAZA (SCFE) YAKUTANA ARUSHA
Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Fedha na Uchumi (SCFEA) pamoja na Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Mashauriano ya Kibajeti umefanyika jijini Arusha tarehe 7 Mei 2021 huku Mawaziri hao wakikubaliana na hoja ya kuiboresha Tume ya Kiswahili ili kuiwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi badala ya kuivunja.
Awali hoja ya kuivunja Tume ya Kiswahili iliwasilishwa kupitia ripoti ya mshauri mwelekezi na kuungwa mkono na takriban Nchi zote Wanachama isipokuwa Tanzania kama moja ya mikakati ya kupunguza gharama za uendeshaji ndani ya Jumuiya.
Hata hivyo,nchi hizo ziliafiki kwa kauli moja hoja zilizolizotolewa na Tanzania kuhusu umuhimu wa Tume hiyo.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo ambaye pia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba alieleza umuhimu wa Tume hiyo na kwamba ni kielelezo pekee muhimu cha Jumuiya na kuwataka kuunga mkono hoja ya kuiboresha na kuiimarisha ili iendelee kutekeleza majukumu yake kikamilifu
Post a Comment