MWINYI AHUDHURIA MKUTANO WA (SEDTS)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ahudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC Extraordinary Double Troika Summit). kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mkutano huo ulifanyika tarehe 27 Mei 2021 jijini Maputo ulihudhiriwa pia na Rais wa Botswana, Malawi, Afrika ya Kusini, Zimbabwe na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi ambae ni mwenyeji na Mwenyekiti wa SADC.
Mkutano huo ulipokea taarifa za Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama kuhusu hali ya usalama katika eneo husika la kaskazini mwa Msumbiji, Cabo Delgado. Vile vile, wajumbe wa mkutano huo waliwahakikishia wananchi wa Msumbiji kuendelea na juhudi za kulinda na kudumisha amani dhidi ya ugaidi nchini pamoja Nchi wanachama wa SADC.

Post a Comment