MWINYI AWATAKA MASJID TAQWA KUSHIRIKIANA
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhadj Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameitaka Kamati ya Msikiti wa Masjid Taqwa kushirikiana na waumin wa mskiti huo katika utatuzi wa changamoto mbali mbali zinazoikabili jamii.
Alhadj Dk.Mwinyi ametowa wito huo katika Ufunguzi wa msikiti mkuu wa Ijumaa wa ‘Masjid Taqwa’ uliopo Bambi Mkoa Kusini Unguja, uliojengwa kwa mashirikiano kati ya wananchi na Mfadhili.
Amewataka waumini hao kuutumia msikiti huo kama kituo cha kujifunza na kuzungumzia matatizo yanayoikabili jamii, kama vile changamoto za imaisha zinazowahusu mayatima, wajane pamoja na vitendo vya udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto.
Alisema mbali na Ibada ya swala, pia kuna umuhimu wa kuendeleza na kuutumia msikiti huo katika mambo mbali mbali, kwa mujibu wa mafunzo ya Mtume Muhammad (SAW).
Alhadj Dk. Mwinyi alisiitiza umuhimu wa waumini wa msikiti huo kuutunza ili uweze kudumu kwa miaka mingi ijayo.
Aidha, aliwaeleza waumini wa msikiti huo wajibu walionao katika kufanya mambo mema ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya akhera yao, akibainisha kila muumini ana nafasi ya kuimarisha msikiti huo katika matunzo, ikiwemo kusaidia huduma za maji, umeme au kuufanyia matengenezo madogo madogo.

Post a Comment