MANARA: BUNGE LIINGILIE KATI
Kabla ya jambo lolote lile kuendelea iundwe Kamati ya kibunge ijiridhishe kuhusu jambo liliotokea leo,ambalo limeacha maumivu makubwa Kwa Washabiki wa soka nchini zaidi ya elfu arobaini ambao walishalipa viingilio vyao il kuangalia mechi hyo,lakini pia liliochafua taswira ya nchi kimataifa ukizingatia nchi nyingi za Afrika zilikuwa zimejiandaa kuangalia game hii!!
Baadhi ya hadidu rejea za tume hyo huru ziwe hz!!
Nn kilisababisha mechi hii kusogezwa mbele Kwa masaa mawili?
Why game Yanga na Azam pamoja Yanga na Biashara Mara ambazo nazo zilisogezwa mbele masaa mawili zilichezwa ila hii ya leo imeshindikana kuchezwa?
Uwazi wa kile kilichosababisha mechi isogezwe mbele Kwa masaa mawili na kwa nn Yanga muda mchache baada ya taarifa hyo kutolewa walitoa taarifa ya kuonyesha kutaka kugomea hyo mechi?
Je kwa nn ugomeaji huu uwe leo na usiwe ktk mechi za Azam au Biashara?
Na kama Serikali ilikuwa na sababu za msingi za kusogeza mbele muda wa mechi Kisha kuiarifu Tff na Shirikisho hilo kuviandikia vilabu vyote barua,,Kwa nn Yanga pekee wagomee? Na kama wamegomea why Simba haikupewa ushindi?
Je hakukuwa na mbinu ya makusudi ya kuhairisha hii mechi?
Kama ilikuwepo nn kitaendelea?
Nani atalipa gharama ambazo klabu zimeingia kujiandaa na mechi hii na nani atalipia gharama za Watanzania waliolipa viingilio vyao sambamba na gharama kwa wale waliotoka nje ya Dar?
Hil jambo lisichukuliwe kirahisi rahisi maana limeacha maswali mengi ambayo Watanzania waliolipa viingilio vyao na wale walionunua vifurushi vya Azam tv wanapaswa kujua, lakini pia limeitia doa ligi yetu ambayo kwenye siku za Karibuni imekuwa maarufu kote barani Afrika,,
Bunge la watu linao wajibu wa kusimamia kero za watu kama hz za leo,,,ni wao pekee kwa sasa wanaweza kuja na majawabu sahihi juu ya kadhia hii iliyowaumiza Watanzania wengi.
Post a Comment