MAANA YA UPENDO

*HIKI KITU _UPENDO_ NI NINI?* Jaribio kupima ufahamu wako kuhusu upendo.
Jibu Ndio(N) au Hapana (H) Kisha rekodi majibu. Ukimaliza nyosha mikono.Uwe mwaminifu sitaona ulicho jaza nitakupa majibu ujisahishe mwenyewe.
 MASWALI:
1.Wadada hupenda haraka kuliko wakaka. (N/H)

2.Ukiupata upendo wa kweli utajua kuwa ni kitu halisi.[N/H]

3.Mhemko na upendo wa kweli ni tofauti sana kiasi kwamba ni rahisi kutofautisha. [N/H]

4.Tamaa/mvuto wa kingono unaweza kuwepo katika upendo Kama ulivyo katika Mihemko(infatuation).[N/H]

5.Mdada anapokuwa katika upendo , anakuwa na mapenzi kuliko mkaka.[N/H]

6.Moja ya njia bora kabisa za kupata upendo ni kufanya urafiki na mtu kwa muda mrefu.[N/H]

7.Kama wewe na mwenzio mmepata upendo wa kweli, _Hamtarumbana kamwe_ 🥷🏼. [N/H]

8.Inawezekana kupenda mtu zaidi ya mmoja kwa wakati huohuo(at the same time).[N/H]

9.Mhemko mkali 🔥wa ngono ni ishara ya upendo wa kweli.[N/H]

10.Kupata ukubali wa familia na marafiki ni moja ya mambo muhimu sana katika kuleta furaha ya ndoa yako hapo mbeleni . [N/H]

11.Shauku ya kuwa pamoja _muda wote_inamaanisha mmepata upendo wa kweli.[N/H]

12. _Upendo wa papo_ _hapo_(mf.umekutana na mtu kwa mara ya kwanza ...halafu ndio🔥🫀) ni aina ya upendo unaodumu sana.[N/F]

13.Inawezekana wenzi kuupata upendo wa kweli baada ya kuwa pamoja kwa miezi 6. [N/H]

14.Inaruhusiwa kwa wenzi kufanya _ngono kabla ya ndoa_ ..ikiwa watakuwa na *uhakika* Kwamba wameupata upendo wa kweli mwishowe.[N/H]

15.Upendo wa papo hapo (love at first sight)unawezekana *ikiwa(* wewe) umefikia umri wa ukomavu.[N/H]

16.Wale ambao wamekuwa katika mahusiano kwa miaka 2 au zaidi _hawahitaji mashauri kabla ya ndoa_ .[N/H]

17.Pale wenzi wapatapo pendo la kweli (kinyume cha Mihemko tu) wataweza kushinda *kila kikwazo* kizuiacho njia yao ya furaha.[N/H]

18.Ukiwa mwangalifu vya kutosha , _utagundua mapema_ kuwa mwenzio anakuwa mkweli kabisa kwako au la.[N/H]

19.Kama umeupata upendo wa kweli *Haijalishi* Kama wazazi wako wanamkubali mwenzio au la. [N/H]

20.Mungu ametuumbia mtu special kwa kila mmoja wetu , na kupitia maombi na kutafuta , nitaongozwa kwa mtu huyu.[N/H]



*PMC 360°©2021™*

No comments