FOMU ZA MAOMBI YA LESENI KUTOLEWA MEI 15

KUTOKA TFF;
Fomu za maombi ya leseni za Klabu msimu wa 2021/2022 kwa Klabu za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili zitaanza kutolewa Mei 15, 2021.

Fomu zinapatikana Makao Makuu ya TFF, Karume, Ilala kwenye Ofisi ya Meneja wa Leseni za Klabu bila malipo yoyote, pia unaweza kupakua kwenye tovuti yetu www.tff.or.tz.

Mwisho wa zoezi la kurudisha fomu itakuwa Julai 15, 2021.

Kwa msimu wa 2021/2022 Klabu yoyote itakayokuwa inadaiwa na mchezaji haitapatiwa leseni ya kushiriki Ligi na kwa Klabu itakayoshiriki
mashindano ya CAF, Kocha Mkuu ni lazima awe na leseni A ya CAF na Kocha Msaidizi awe na leseni B ya CAF.

No comments