FASHION SAKALA KUTUA RANGERS YA GERALD
FOWADI Fashion Sakala amesema kwamba uhamisho wake kutoka kambini mwa KV Oostende ya Ubelgiji hadi Rangers ya Ligi Kuu ya Scotland “ni kutimia kwa ndoto yake katika soka.
Nyota huyo raia wa Zambia mwenye umri wa miaka 24, ametia saini mkataba wa awali wa miaka minne na anatarajiwa kutua jijini Ibrox, Scotland kufikia mwisho wa wiki baada ya kupata kibali cha kufanya kazi nchini Scotland.
Sakala ameifungia Oostende jumla ya mabao 13 kutokana na mechi 29 katika Ligi Kuu ya Ubelgiji msimu huu wa 2020-21.
Kulingana na yeye, Rangers ya kocha Steven Gerrard ni miongoni mwa vikosi bora zaidi duniani.
“Ni kikosi kinachojivunia idadi kubwa ya mashabiki na historia ndefu ya mafanikio katika soka ya Scotland. Naamini kwamba kujiunga kwangu na klabu hii kutanikuza zaidi kisoka kadri ninavyolenga pia kuwa sehemu ya historia ya ufanisi wa timu huu maarufu,” akasema Sakala.
Sakala aliingia katika sajili rasmi ya Oestende miaka mitatu iliyopita baada ya kuagana na klabu ya Spartak Moscow ya Ligi Kuu ya Urusi. Tangu wakati huo, anajivunia kufungia Oostende jumla ya magoli 26 kutokana na mechi 90 huku akishirikiana vilivyo na kiungo raia wa Scotland, Jack Hendry anayechezea Oostende kwa mkopo kutoka Celtic.
Baada ya kukamilisha kampeni za muhula huu katika nafasi ya tano, Oostende watashiriki mchujo wa kufuzu kwa soka ya Europa League msimu ujao wa 2021-22.
Sakala ameichezea timu ya taifa ya Zambia almaarufu ‘Chipolopolo’ mara 11 na akaifungia kikosi hicho bao moja. Mchuano wake wa kwanza ndani ya jezi ya Chipolopolo ilikuwa Septemba 2017

Post a Comment