BARUA YA YANGA SC KWA UMMA NA KWA TFF
Uongozi wa Klabu ya Yanga, umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya mabadiliko ya muda wa Mchezo baina ya Simba SC na Yanga SC
yaliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutoka saa 11:00 jioni hadi saa 1:00 usiku.
Mabadiliko haya ni kinyume na kanuni ya 15 (10) za Ligi Kuu inayohusu taratibu za mchezo ambayo inasema "Mabadiliko yoyote ya muda wa
kuanza mchezo yatajulishwa ipasavyo kwa pande zote husika za mchezo angalau saa 24 kabla ya muda wa awali."
Hivyo basi uongozi wa Yanga unapinga mabadiliko haya hivyo, Yanga itapeleka Timu Uwanjani kwa muda wa awali wa saa 11:00 jioni. Uongozi wa Yanga unaitaka Bodi ya Ligi na TFF kuendesha Ligi kwa kuzingatia na kuheshimu kanuni zilizowekwa.
Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano
Yanga SC.
Post a Comment