AMKA NA BWANA LEO 6

KESHA LA ASUBUHI

ALHAMISI, MEI, 6, 2021
SOMO: MAMBO MUHIMU YA UKOMBOZI 

Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru. 

Waefeso 5:8. 



Yeye ambaye aliamuru nuru ing’ae gizani anatoa nuru katika akili ya kila mtu ambaye atamtazama vizuri, akimpenda sana, akionesha imani isiyoyumba na kumwamini. Nuru yake inang’aa katika vyumba vya akili na katika hekalu la moyo. Moyo unajazwa na nuru ya maarifa ya uzuri ambao unang’aa katika uso wa Yesu Kristo. Na kwa nuru hii unakuja ufahamu wa kiroho.... 



Tukiukubali kwa hiari ushahidi wa ukweli, na kutembea katika nuru ambayo inang’aa katika njia zetu, bado tunapokea nuru kubwa. Kupitia nguvu ya udhihirishaji wa utukufu wa kiungu, daima tunakua katika ufahamu wa kiroho. 



Maarifa ya Kristo kuhusu ukweli ulikuwa wa moja kwa moja, chanya, usio na kivuli. Kwa kadiri ambavyo mwanadamu anakuwa karibu na Yesu Kristo, ndivyo atakuwa mwangalifu zaidi kuwatendea wanadamu wenzake kwa heshima, kwa ukarimu na kwa haki. Amejifunza kwa Kristo, na anafuata mfano Wake katika neno na vitendo. Kwa imani ameunganishwa na Kristo. “Sisi ni watenda kazi pamoja na Mungu” (1 Wakorintho 3:9) .... 



Ombi la Kristo lilikuwa ni kwa ajili ya umoja miongoni mwa wafuasi Wake. Umoja huu ni ushahidi unaopaswa kuisadikisha dunia kwamba Mungu amemtuma Mwana Wake kuwaokoa wenye dhambi. Tunamtumikia Kristo kwa kudhihirisha ukweli, usafi, upendo mtakatifu kwa wengine. Wale ambao wamechaguliwa kujihusisha na taasisi za Bwana wanapaswa kujitolea, watu wa kujikana nafsi, watu wa kujitoa mhanga, wakiishi si kwa kujifurahisha wenyewe bali kumpendeza Bwana. Hawa ni watu ambao wataleta heshima katika taasisi za Bwana. 



Kumfahamu Mungu na Kristo ni jambo muhimu katika wokovu. Tunapoteza mambo mengi kila siku ambapo hatujifunzi zaidi kuhusu upole na unyenyekevu wa Kristo. Wale wanaojifunza kuhusu Kristo wanapata elimu ya juu kabisa. Kupitia imani na kuitegemea imani iokoayo ya Kristo, wanakuwa katika maarifa na hekima. Wanampenda na kumtukuza Mwokozi.... 



Wale ambao wameokolewa ni lazima waifanye iwe shughuli yao ya kila siku kupokea neema kutoka kwa Mungu, wala si kukaa katika ubinafsi, bali kuisambaza kwa ajili ya kuwabariki wale ambao wanahusiana nao, ili kuwasaidia katika kupata elimu ya mambo ya kiroho.



—Letter 191, Mei 6, 1901

No comments