AMKA NA BWANA LEO 28
KESHA LA ASUBUHI
IJUMAA, MEI, 28, 2021
SOMO: KRISTO AKAAYE NDANI
Yeye asemaye kwamba yumo nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa. Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.
1 Yohana 2: 9, 10.
Usiku uliopita niliota kwamba kundi dogo lilikuwa limekusanyika pamoja kwa ajili ya mkutano wa kidini. Kulikuwa na mtu ambaye alikuja na akakaa kwenye kona yenye giza, ambapo asingeonekana sana. Hakukuwa na roho ya uhuru. Roho ya Bwana ilitamalaki. Mzee wa kanisa alitoa maoni fulani. Alionekana akijaribu kumuumiza mtu. Niliona huzuni usoni pa yule mgeni. Ilikuwa dhahiri kwamba hakukuwa na upendo wa Yesu katika mioyo ya wale ambao walidai kuuamini ukweli wa Yesu, na kwa hakika, matokeo yake, hakukuwa na roho ya Kristo na upungufu mkubwa wa kumpenda Mungu na watu wengine katika mawazo na hisia. Kusanyiko la pamoja halikuwa likimfariji mtu yeyote.
Mkutano ulipokuwa unakaribia kufungwa, mgeni yule alisimama na kwa sauti ambayo ilijaa huzuni na machozi, aliwaambia kwamba walikuwa na uhitaji mkubwa wa upendo wa Kristo, katika roho zao na katika uzoefu wao, ambao ulikuwepo kwa kiwango kikubwa kwenye kila moyo ambapo Kristo alifanya makao Yake. Kila moyo ambao umehuishwa na Roho wa Mungu hautampenda Mungu tu bali utampenda ndugu yake, na ikiwa huyo ndugu amefanya makosa, ikiwa amekosea, anapaswa kushughulikiwa sawasawa na mpango wa injili. Kila hatua inapaswa ifuatwe kulingana na maelekezo yaliyotolewa katika Neno la Mungu.
Alisema, “Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.” (Wagalatia 6:1). “Je, hukumbuki ombi la Kristo kabla hajawaacha wanafunzi wake na kwenda katika pambano lake la muda mrefu lenye maumivu makali katika bustani ya Gethsemane, kabla hajasalitiwa, kabla hajahukumiwa, na kusulubiwa?” (Yohana 17:15—23)....
Uwe mwangalifu kwa jinsi unavyoshughulika na wale walionunuliwa kwa damu ya Kristo. Kutakuwa na haja ya kukemea kwa wazi na kwa uaminifu matendo ya uovu, lakini yule anayechukua jukumu hili ajue kwamba hajatengwa na Kristo kwa matendo maovu yeye mwenyewe. Anapaswa kuwa mtu wa kiroho na kumrejesha huyo mtu kwa roho ya upole....
Roho na tabia ya Kristo zinadhihirishwa katika wateule wa Mungu, kwa mazungumzo ya kimbingu, upole wao, tabia yao isiyokuwa na waa. Kadiri ya watu wengi wanapoongozwa na Roho wa Mungu, ni wana wa Mungu.
—Manuscript 32, Mei 28, 1887,, shajara, "Ziara ya Ujerumani."
Post a Comment