MAKATIBU WAKUU WA ELIMU NA TAMISEMI WAKUTANA (KIKAO)
Kamati ya Makatibu Wakuu wa Wizara zenye dhamana ya Elimu, Michezo na TAMISEMI tarehe 27 April 2021 na baadhi ya Watendaji wa Sekta hizo wamefanya kikao kazi kujadili utekelezaji wa maelekezo ya Mawaziri wenye dhamana hizo yaliyotolewa Februari 8, mwaka huu kwa lengo la kuandaa mkakati wa utekelezaji wa masuala mbalimbali ya uimarishaji wa somo la Elimu kwa Michezo na Michezo kwenye Shule za Msingi na Sekondari hapa nchini. Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za TAMISEMI zilizopo Mtumba jijini Dodoma.
Post a Comment