FIZIKIA YA KUSIKIA
*FIZIKIA YA KUSIKILIZA*
Tumekuwa tukijifunza kuhusu Mawasiliano Kama 🫀wa Mahusiano , na tumegundua kuwa mapigo ya moyo huu ni *KUELEWA(Understanding).* Tunaposikiliza ndipo tunaelewa. Leo , tunakamilisha mada hii kwa kujifunza _Namna ya Kusikiliza._
*Assume kuwa unayemsikiliza anajua kitu fulani usichokijua* : _Wakati mwingine inakubidi ubadili vile unavyoelewa kila kitu Ili uelewe vema kitu kimoja_.Unapojikita kwenye mazungumzo halisi , unaongea na kusikiliza- lakini muda mwingi unakuwa unasikiliza. Kusikiliza ni kuwa makini. Utashangazwa mambo watu watakayokuambia ikiwa *utawasikiliza.Wakati mwingine watakuambia kile kinachowasumbua.Wakati mwingine watakuambia hata jinsi walivyopanga kulitatua jambo hilo.Kuna wakati ambao kuwasikiliza kwako kunakusaidia kutatua kile kinachokusumbua wewe mwenyewe* .[Jordan B. Peterson: 12 RULES FOR LIFE]
*Epuka kubadili mood kwa ghafla:* unapokuwa ukisikiliza epuka kubadili mood kwa ghafla.Hii itashusha uwezo wako wa kuvaa viatu vya mwingine na hutamuelewa. Itamfanya Mzungumzaji aache kuwasiliana na kuanza kujihami.
*Sikiliza kwa* 🫀🧠👀: Tulia ,tena uwepo kabisa.Kama unaona ujatulia kwa wakati huo...panga muda mwingine ambapo unaweza Kusikiliza hasa. Tafiti zinaonyesha kuwa inatuchukua dk 21 kurudi katika umakini uliyokuwa nao kabla hujahamisha umakini wako. Mfano. Ulikuwa unasoma ghafla ukaanza kuchat....kurudisha umakini wa awali itachukua dk......(jaza nafasi zilizo wazi).
*Epuka Ujuaji* : ```Mjuaji(a Know-it-all) ni mtu anayejua kitu isipokuwa jinsi``` *anavyokera* .-Demitri Martin.
°Tafuta kuelewa *kwanza , kabla* hujataka kueleweka.
° *Jifunze kusikia visivyosemwa/ maneno yaliyomezwa* : mtu anaweza kuwa anapitia nyakati ngumu lakini akawa hasemi au anameza kitu ambacho ingempasa kukitema Ili apone.Jifunze kusoma dalili na uwepo kwa ajili yao.
° *Uliza Maswali* :
Uliza lakini Uwe na busara , kuna tofauti Kati ya mazungumzo na interview.ULIZA ! TULIA! SIKILIZA! Aulizaye ndiye atawalaye muelekeo wa mazungumzo.Epuka ubishi... _wakati mwingine kitendo kidogo Cha kutamka swali kinaweza kukufanya upate majibu haraka kuliko uliyemuuliza. Inatokea sana_
*Jifunze kufupisha* : Rudia na kufupisha kile ulichosikia kwa maneno yako mwenyewe....maneno ya dk5 yanaweza kufupisha kwa sentensi tatu.
John: Hi! James..makambi yalikuwaje?.....James : Yaani sio poa..yalifana sana..duh..tulifurahi mno.
John: ayaah! Nimepitwa na mengi... lakini James huwezi kunielezea kifupi maarifa uliyoyapata.
James: John , umepitwa mwanangu....lile lile kambi lilipendeza sana🥱🤔. *Kama huwezi kurudia kwa ufupi ulichosikia , basi hukusikiliza na hivyo hukuelewa* .
° *Tumia viitikio:* mfano kutikisa kichwa. Kuwa makini usiwe mtu wa ndio Mzee kwa kila kitu. Mzungumzaji anaweza kudhani unakubali kumbe unaelewa tu..
° *Wambie uchofikiri wanamaanisha na ruhusu wakurekebishe* . _Ni jambo la Hekima sana kujua kile wasichomaanisha pia. Katika Mawasiliano kile mtu asichomaanisha ni muhimu sawa na Kile anachomaanisha_ .
*PMC 360°©2021™*
Post a Comment