AMKA NA BWANA LEO 4

KESHA LA ASUBUHI

JUMAPILI, APRILI, 4, 2021
SOMO: UTUKUFU USIOELEZEKA 

Maana tangu zamani za kale watu hawakusikia, wala kufahamu kwa masikio, wala jicho halikuona Mungu, ila wewe, atendaye mambo kwa ajili yake amngojaye. 


Isaya 64:4 



[Katika kujibu maombi ya Bibi Stewart, msanii aliyemwomba Ellen White kuandika juu ya maelezo ya Yerusalemu mpya]



Umeeleza matamanio yako kwangu kuelezea mambo yanayohusiana na Yerusalemu mpya. Nilikataa kwa wema kufanya jambo la namna hiyo. Nguvu zangu zisingetosha kufanya hivyo au hata kudiriki kujaribu, na ninakushauri usifanye jaribio lolote la kuwa na kiwakilishi chenye kumfanya mtu adhani kuwa ni kiwakilishi cha Yerusalemu mpya. Umahiri wa juu zaidi wa uwakilishi wa Yerusalem Mpya ni kutojaribu kuuwasilisha. 



Mtu yeyote anayejishughulisha kuelezea utukufu usiotamkika wa mambo yajayo ya ulimwengu usioonekana ni vyema akafanya hivyo kwa kunukuu maneno ya Paulo “jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.” 1 Wakorintho 2:9). Ninahisi kuwa wengi wanayachukulia mambo matakatifu kana kwamba uwezo wao wenye ukomo unaweza kuyaelewa... 



Kuna idadi kubwa ya watu ambao wanatembea katika eneo takatifu wakiwa na miguu isiyotakaswa jambo ambalo tunajihadhari nalo, hata katika kauli tunazoziwasilisha kwao kuhusiana na vitu vitakatifu vya milele, kwa sababu mawazo ya kawaida na yenye kikomo huchanganywa na yaliyo matukufu na matakatifu. Mwanadamu anaweza kujaribu kwa kutumia nguvu alizokabidhiwa pamoja na elimu kuwakilisha kitu fulani cha mbinguni na kuishia kuharibu kila kitu. 



Uwezo wako kama msanii utakapotanuliwa mpaka kufikia kiwango chake cha juu kabisa utaanguka chini na kuzirai na utachoka kutafuta kuyaelewa mambo ya ulimwengu usioonekana, na bado ni kweli kuwa kuna umilele ng’ambo yake. Kwa kauli hizi utaniwia radhi kwa kutokujaribu kuchora kitu chochote kuhusiana na kazi ya Bwana ambaye ndiye Msanifu Mkuu. 



Hebu fikra za watu kwa kiasi kikubwa ziwe juu ya kutafakari utukufu wa Yerusalemu Mpya, na bado hapo watakuwa wangali katika kingo za utukufu wa milele uzidio watakaopata washindi waaminifu. Vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu. Hili ni jibu bora sana ninaloweza kulitoa kwa swali lako. 



—Letter 54, April 4, 1886,, to Sister Stewart

No comments