AMKA NA BWANA LEO 2

KESHA LA ASUBUHI

IJUMAA, APRILI, 2, 2021
SOMO: TATHMINI YA KIMBINGU 

Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. 

Warumi 12:1 



Kuna upimaji wa tabia unaoendelea wakati wote. Malaika wa Mungu wanapima maadili yako na kuyakinisha mahitaji yako na kuipeleka kesi yako mbele za Mungu. Ni kwa bidii kiasi gani tunatakiwa kukazana kufikia nia ya Roho wa Mungu. Tungekuwa na shukrani kiasi gani kwamba msaada huo umewekwa kwake Yeye mwenye uwezo wa kuokoa!....



Je unadhihirisha hasira na kutamka maneno kwa papara? Je umejaa hali ya kujiamini? je una mawazo na matendo ya kuwaka tamaa? Je, unafanya mambo dhahiri kinyume na kusudi la Mungu? Je, unamwibia Baba yako wa mbinguni kwa kumzuilia vipaji na moyo wako? Kwanini usikome kufanya hivyo? Kwanini usijitoe kikamilifu kwa Mungu? Atakuangazia nuru Yake na kukupa amani nawe utaonja raha ya wokovu Wake. 



Usimletee Mungu tena sadaka kilema yenye kasoro. Nguvu zako kiakili na kimwili zimedhoofishwa na uasi wako; lakini sadaka ya aina hiyo haikubaliki mbinguni. Kwanini usije ukaponywa udhaifu wako na kuitoa sadaka hai takatifu isiyo na mawaa? Je! umekuwa ukimwibia Mungu zaka na sadaka? Haya ni maelekezo anayoyatoa Mungu kwa ajili yako, “ Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kawamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.” (Malaki 3:10) Kwanini usiamini Neno la Bwana? Ni fadhila kwetu kupata uzoefu wa furaha ya Kristo. 



Litakuwa ni jambo gumu sana kuwashawishi wale walioonja ujuzi kamili wa Kristo, kwamba Yeye kama mzizi katika nchi kavu bila umbo wala uzuri ” na ambaye “Ndiye mzuri sana pia pia” (Wimbo Ulio Bora 5:10,16) Ninampenda! ninampenda Yeye! Kwa Yesu ninaona uzuri usioelezeka. Ndani yake ninaona kila kitu kinachotamaniwa na wana wa wanadamu. Hebu tuje kwa “Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” (Yohana 1:29). Hebu kupitia stahili na haki Yake tupate kufaa kwa ajili ya mbingu. Yesu hataudharau moyo uliovunjika na wenye toba ya kweli. 

No comments