TETESI ZA SOKA KIMATAIFA
Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 33, atacheza misimu miwili zaidi barani Ulaya kabla ya kujiunga na Inter Miami ya MSL, huku uwezo wa mchezaji huyo kuendelea kusalia Barcelona hata baada ta msimu huu ukibashiriwa kuwa kwa asilimia 50 - 50. (Cadena Ser - in Spanish)
Chelsea inamnyatia winga wa Bayern Munich raia wa Ufaransa Kingsley Coman, 24, kama mwenye uwezekano wa kuchukua nafasi ya Christian Pulisic, wakati ambapo mchezaji huyo wa miaka, 22, raia wa Marekani ameonesha kuwa anataka kuondoka Stamford Bridge. (Mail)
Arsenal, West Ham, Everton na Brighton wanafanya mazungumzo ya kumsajili mlinzi wa Scotland,18, Ibane Bowat kutoka Fulham. (TeamTalk)
Ajenti wa Gianluigi Donnarumma, Mino Raiola inasemekana kwamba alianza mazungumzo na Chelsea na Manchester United kuhusu mlindalango wa AC Milan, 22. Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia aliye San Siro utamalizika msimu huu. (Transfer Window Podcast, via Football London)
Kiungo wa kati Manchester United Nemanja Matic, 32, amesema atafikiria kurejea Benfica ikiwa kuna atakayemuhitaji, ingawa mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia anasisitiza kwamba ni mwenye furaha Old Trafford. (Sport TV, via Sun)
Wolves ina nafasi ya kufanya majadiliano ikiwa itaamua kufikia makubaliano ya kudumu na mshambuliaji wa Brazil Willian Jose,29, ambaye yuko kwa mkopo kutoka kwa Real Sociedad, beki wa Ufaransa Rayan Ait-Nouri, 19, ambaye yuko kwa mkopo kutoka kwa Angers, na kiungo wa kati wa Ureno, Vitinha, 21 kutoka Porto. (Express and Star)
Barcelona itatoa mkataba kwa kiungo wa kati wa Uholanzi, 30, Georginio Wijnaldum, ambaye anatarajiwa kuondoka Liverpool kwa uhamisho wa bure wakati mkataba wake utakapomalizika mwisho wa msimu. (Football Insider)
Inter Milan pia imefanya mazungumzo na ajenti wa Wijnaldum lakini yamekwama kwasababu klabu hiyo inaendeleza malengo mengine. (Calciomercato - in Italian)
Joan Laporta, ambaye alitajwa kama rais wa Barcelona kwa mara ya pili baada ya kushinda uchaguzi wa klabu hiyo Jumapili, amesema kuwa anataka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 20, na atukuwa mlengwa wake mkuu katika kipindi cha msimu. Laporta anataka Barca iwe na raia huyo wa Norway na Lionel Messi, ambaye mkataba wake unamalizika msimu huu. (Diario AS - in Spanish)
Aliyekuwa kocha wa Chelsea Maurizio Sarri anapangiwa kurejea Napoli kama kocha, hatua ambayo huenda ikachangia kiungo wa kati wa Chelsea Jorginho pia arejee katika klabu ya Italia. (Radio Kiss Kiss, via Express)
Juventus pia inafikiria kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia, 29. (Tuttosport - in Italian)
Mlinzi Konstantinos Mavropanos wa Arsenal, 23, raia wa Ugiriki ambaye amemvutia kocha wa Stuttgart wakati wa kipindi chake cha mkopo hayuko tayari kuondoka Gunners. (Bild, via Mirror)
Ligi ya Primia inaandikia vilabu kuwauliza maoni makocha, wakurugenzi wa soka na manahodha juu ya VAR ikiwa na mtazamo wa kuborosha teknolojia hiyo msimu ujao. (Mail)
Post a Comment