mafunzo ya watu wazima leo mchana 6
LESONI, MACHI 6
SOMO: KUENDELEZA UPENDO
SABATO MCHANA
Somo la Juma Hili: Isaya 55: 1—7; Isaya 55: 6—13; Isaya 58: 1—12; Isaya 58:13, 14.
Fungu la Kukariri: "Na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri." (Isaya 58:10).
Kiongozi mmoja wa ibada wa Kiyahudi pamoja na mkewe ambao waliishi Lincoln, Nebraska, walianza kupokea simu za vitisho na matusi. Wakagundua kuwa simu hizo zilitoka kwa kiongozi wa kikundi chenye chuki cha Wamarekani, Ku Klux Klan. Kwa kujua utambulisho wake, wangeweza kumripoti kwa polisi. Lakini waliamua kutumia njia ya msingi zaidi. Walipogundua kuwa alikuwa kilema, walifika mlangoni pake wakiwa na chakula cha jioni chenye kuku! Alishangazwa mno. Chuki yake iliyeyuka mbele ya upendo wao. Wenzi hao walidumu kumtembelea, na urafiki ukakua. Hata akafikiria kuwa Myahudi!
“Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako .... ?” (Isaya 58: 6, 7). Jambo la kinyume, wenzi hao huko Lincoln walifanya mfungo kama huo kwa kushiriki karamu yao na mtaabishaji mwenye njaa, na hivyo kumweka huru kutoka katika vifungo vyake vya chuki isiostahili!
Hebu tujifunze zaidi kuhusu kanuni hii muhimu ya kiroho kama inavyoelezwa na nabii Isaya.
Jifunze somo la juma hili kwa maandalizi ya Sabato ya Machi 13.
Post a Comment