amka na Bwana leo 7
KESHA LA ASUBUHI
Jumamosi 06/03/2021
*FUNGUA MLANGO*
*Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.* *Ufunuo 3:20*
*Wakati moyo utakuwa bila kujiona wa thamani binafsi, mlango utafunguliwa kwa ajili ya Kristo, kwa kuwa utatambua kubisha kwake.* Lakini usipofagia takataka zinazomfungia Yesu nje; hataweza kuingia, kwa kuwa halazimishi kuingia.
Katika njozi za usiku nimekuwa nikibeba ushuhuda wa dhati kwamba Bwana Yesu atapatikana kwa wale wanaomtafuta kwa moyo wote, na kumshikilia kwa imani. Nilikuwa ninazungumza nanyi kwa mkazo wa dhati. *Hebu jibuni ombi la Yesu kwa ajili ya umoja, na kuweka kando mashaka ambayo Shetani anatumia kuwapotosha. Mfukuzeni adui, na kisha Roho wa Bwana atainua kwa ajili yenu kiwango kinyume cha adui.*
Ustawi wa nafsi hutegemea kafara ya upatanisho ya Kristo. Alikuja katika ulimwengu huu kupata msamaha kwa niaba yetu. Kazi yetu ya kwanza ni kupambania kwa bidii sana baraka za kiroho, ili kwamba tuweze kudumu kuwa watiifu na wakweli katikati ya maasi ya siku hizi za mwisho - kuhifadhiwa toka katika kukubaliana hata kidogo na hila za Shetani. Ni jukumu la kila mmoja kutengeneza njia nyoofu kwa ajili ya miguu yake, aliye mlemavu asije akakoseshwa njia. *Hatuna muda wa kupoteza. Ustawi wa nafsi hutegemea umoja ambao Kristo aliomba uwepo miongoni mwa wale wanaomwamini. Wanapaswa kuwa wamoja pamoja Naye kama vile yeye alivyo umoja na Baba* Tunavyosogea mbali toka kwa kila mmoja sio mpango wa Mungu, bali mpango wa adui mwerevu.
Tunapaswa kuwa macho na wale wanaokana uzoefu wao uliopita, na wale, kwa udanganyifu wa hila, wanaweza kudanganya kama yumkini hata walio wateule. *Yeye ambaye ni Wakili wetu katika nyua za mbinguni anazifahamu kila aina ya hila zidanganyazo za wale wazifanyao hii kazi.* Wale wanaojiengua toka katika imani wako kazini kudharau ujasiri wa wengine, na wamekuwa hivyo kazini kwa miaka. Maonyo yetu hutujia toka kwake anayetujali kwa kuwa huona hatari zetu, na kula njama kwao wale wanaopingana na kweli yake.
*Yeye ambaye ni Mwombezi wetu katika nyua za mbinguni atawatakasa watu wake. Kristo atawakamilisha watakatifu wake.*
*MUNGU ATUBARIKI TUNAPOTAFAKARI NENO LAKE*
Post a Comment