mafunzo ya watu wazima leo

LESONI, MACHI 2

SOMO: NI NANI ALIYESADIKI? (ISA. 52:13—53:12)



Katika Isaya 52:13 Mtumishi wa Mungu anaadhimishwa sana, lakini bila tahadhari, fungu linalofuata huelezea mwonekano wake kama ulioharibiwa sana hawezi kutambuliwa kama mmoja wa “wana wa wanadamu.” Agano Jipya huelezea sababu zilizosababisha kuharibika kwa mwonekano wa Yesu, ikijumuisha kupigwa mijeledi, taji ya miiba, kusulibiwa, lakini zaidi ya yote, kubeba dhambi za jamii ya wanadamu. Dhambi haikukusudiwa kuwa ya asili kwa wanadamu; kuibeba kulimfanya “Mwana wa Adamu” aonekane kama si mwanadamu. 



Linganisha hili na kisa cha Ayubu, ambaye kwa ghafla aliporomoka kutoka katika nafasi ya utajiri mkuu, heshima, na uwezo kufikia kuwa maskini wa kutupwa akikaa katikati ya majivu juu ya ardhi na akiyakuna majipu yake yanayouma kwa kutumia kigae (Ayubu 1, 2). Tofauti ilikuwa kubwa kiasi kwamba hata marafiki wa Ayubu hawakuweza kumtambua mwanzoni (Ayubu 2:12). Swali ni: Kwa nini Ayubu ateseke? Kwa nini lazima Masihi wa Mungu ateseke? Hakuna anayeyastahili. Wote hawana hatia. Kwa nini, basi, kuteseka? 



Soma mafungu ya leo na kuandika mahali ambapo mada ya mateso ya asiye na hatia kwa ajili ya mwenye hatia hujitokeza. Kuna ujumbe gani muhimu hapo kwa ajili yetu?



Yatazame maswali katika Isaya 53:1. Maswali haya husisitiza juu ya changamoto ya kuamini jambo lisiloweza kuaminiwa (linganisha na Yohana 12:37—41) na kutufanya kuketi chini kusikiliza sehemu yote iliyobaki ya simulizi. Lakini maswali humaanisha wito. Katika muktadha huu, kufanana kati ya maswali mawili humaanisha kwamba mkono/uweza wa Bwana wa wokovu (linganisha na Isa. 52:10) umedhihirishwa kwa wale walioiamini taarifa. Je, unataka kupata uzoefu wa uweza wa Mungu unaookoa? Basi iamini taarifa. 



Tazama kwa makini Isaya 53:6. Ujumbe mahsusi hapo ni upi? Fungu hilo husema nini kwako binafsi, kinachopaswa kukupa tumaini licha ya dhambi zako za wakati uliopita na kushindwa?

No comments