mafunzo ya watu wazima leo 5

LESONI, MACHI 5

JIFUNZE ZAIDI:



“Kristo alizibeba dhambi zetu katika mwili wake mwenyewe mtini.... Dhambi ni nini hasa, ikiwa hakuna kiumbe mwenye ukomo angeweza kufanya upatanisho? Laana yake itakuwa nini hasa ikiwa Uungu pekee ungeimaliza? Msalaba wa Kristo unashuhudia kwa kila mtu kwamba adhabu ya dhambi ni mauti.... Ni lazima kuwepo na nguvu fulani ya kisihiri inayoshikilia utambuzi wa kimaadili, ikiwashupaza dhidi ya mvuto wa Roho ya Mungu?” —Ellen G. White, Our High Calling, uk. 44.



“Sheria ya serikali ya Mungu ilipaswa kuadhimishwa kwa kifo cha Mwana pekee wa Mungu. Kristo alibeba hatia ya dhambi za ulimwengu. Utoshelevu wetu unapatikana tu katika kufanyika mwili na kifo cha mwana wa Mungu. Angeteseka, kwa sababu [alitegemezwa] na Uungu. Angestahimili, kwa sababu hakuwa na waa lolote la kutotii au dhambi. Kristo alishinda kwa niaba ya mwanadamu kwa kubeba huko haki ya adhabu. Aliwapatia wanadamu uzima wa milele, wakati akiiadhimisha sheria, na kuifanya iwe yenye heshima.” —Ellen G. White, Selected Messages, book 1, uk. 302. 



MASWALI YA KUJADILI:

1. Isaya 53:7—9 hushuka katika kina cha shimo refu: kifo cha Mtumishi na kuzikwa. Ni nyanja ngapi za haya mafungu zilitimizwa mwishoni mwa maisha ya Yesu? Mat. 26:57—27:60, Mk 14:53—15:46, Lk 22:54—23:53, 9 Yn 18:12—19:42. 



2. Itazame nukuu ya mwisho hapo juu kutoka kwa Ellen G. White kuhusu kifo cha Yesu kuiadhimisha sheria. Anamaanisha nini kwa hilo? Tunaelewaje kifo chake kama uthibitisho wa umilele wa sheria? 


   Muhtasari: Baada ya kusema kuhusu kuzaliwa, utambulisho, na kazi ya Mkombozi aliyetumwa na Mungu, Isaya hatimaye anafunua msiba mkuu unaotupatia tumaini: kufikia, kuokoa, na kuponya watu waliopotea, pamoja na sisi, Mtumishi wa Mungu kwa hiari anabeba mateso na adhabu yetu. 

No comments