amka na Bwaana leo 5
KESHA LA ASUBUHI
IJUMAA, MACHI, 5, 2021
SOMO: ZAIDI YA MANENO
Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
Mithali 4:23
Pasipo utakaso kamili wa maisha, pasipo upole na unyenyekevu wa moyo, wanaodai kuwa wafuasi wa Kristo hawawezi kumheshimu Yeye mbele ya ulimwengu. Ikiwa sifa za Kristo hazifunuliwi maishani mwao, hawawezi kupelekwa katika makao ya mbinguni ambayo ameenda kuwaandalia wale wampendao na kuzishika amri Zake.
Miongoni mwa washiriki wetu wapo wengi ambao, wakati wanapodai kutembea katika njia za Bwana, katika kudai kwao wanaleta njia na tabia za nafsi ambayo hazijaongolewa, na hizi huharibu tabia zao. Mengi ambayo ni upuuzi huletwa katika maisha ya nyumbani na kanisa, kwamba Roho ya Kristo huhuzunishwa. Kuna familia miongoni mwetu ambazo, ikiwa hawataamka toka katika utofauti wao wa kulala, zitapotea; kwa kuwa hawaongolewi siku kwa siku; hawaielewi sayansi ya kiungu ya utauwa wa kweli; na kwa hiyo wao si vyombo ambavyo Bwana anaweza kuvitumia.
Wamemruhusu Shetani kuwa na uongozi na utawala wa maneno na matendo yao, na hawatambui ni madhara mengi kiasi gani wametenda kwa nafsi nyingi kwa kujikweza kwao binafsi. Wameumiza moyo wa Kristo, kwa kuwaumiza wale walionunuliwa kwa damu yake. Nimeambiwa kusema kwa hawa wanaokiri imani pasipo kuongoka, “Chimba kwa kina, na kuweka misingi yenu kwa uimara juu ya Mwamba Kristo Yesu.” Haitoshi sisi kuzungumza kuhusu maisha ya juu. Sababu yetu ya kila siku ni kuwa tafsiri kwa wengine kile maisha ya juu humaanisha....
Maisha yajayo ya umilele ya kila mtu hutegemea, si katika maneno, si katika kukiri imani, bali katika kazi ya dhati. Tunahitaji juhudi za dhati ili kuweza kuutunza moyo kwa bidii zote, huku tukimtazama Yesu kama mwenye kuanzisha na kutimiliza imani yetu. Tunapaswa kuchunga ulimi kaidi; tunapaswa kutafuta fursa za kutenda mema kama Yesu alivyofanya.
Wahubiri wa injili, mhubirini Kristo. Ileteni neema yake ya kimbingu katika maisha na mawazo yenu. Iweni wakweli, na mara zote dumuni chini ya nidhamu ya Neno la Mungu. Ni sharti tuokolewe katika njia aliyoichagua Mungu. Ni lazima tutegemee katika ushauri wake, na kuungana katika kazi zake. Moyo wenye kutubu mara zote huwa mwepesi kuhisi. Wafundisheni kila mtu anayedai kuwa mtoto wa Mungu, kwamba tabia iliojengwa vizuri mara zote itafuata mfano wa Mungu.
Post a Comment