mafunzo ya watu wazima leo 4
LESONI, MACHI 4
SOMO: SADAKA YA FIDIA INAYOBADILISHA (ISA. 53:10—12)
Inamaanisha nini kusema kwamba maisha ya Mtumishi ni “sadaka kwa ajili ya dhambi” (Isa. 53:10)?
Neno la Kiebrania hurejelea “hatia/sadaka ya fidia” (Mambo ya Walawi. 5:14—6:7, Mambo ya Walawi 7:1—7), ambayo ingelipa fidia kwa makosa ya kukusudia dhidi ya watu wengine (Mambo ya Walawi 6:2, 3). Dhambi kama hizi zilibainishwa na Isaya (Isa. 1—3; Isa. 10:1, 2; Isa. 58). Pia, mwenye dhambi sharti amrejeshee aliyemkosea kile alichokuwa amechukua, pamoja na adhabu, kabla ya kutoa sadaka ili kupata msamaha kutoka kwa Mungu (Mambo ya Walawi. 6:4—7; linganisha Mt. 5:23, 24). Kwa habari ya kutumia kitu cha Mungu vibaya kwa kughafilika, sadaka ya fidia huenda Kwake. (Mambo ya Walawi 5:16).
Sasa tunaweza kuielewa Isaya 40:2, ambapo Mungu anawafariji watu wake waliohamishwa kwa kuwaambia wamelipia sadaka ya kutosha kwa fidia ya dhambi zao.
Lakini kufuatia kulipa sadaka ya fidia, lazima kuwe na kafara. Hapa ipo katika Isaya 53: Mtumishi wa Mungu, badala ya kondoo mume, anapelekwa kama kondoo apelekwaye machinjoni (Isa. 53:7) badala ya watu waliopotea (Isa. 53:6)
Ijapokuwa “amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai” (Isa. 53:8, linganisha Dan. 9:26), aliteketezwa kabisa katika kafara iliyowasha mwale wa tumaini kwa ajili yetu, Mtumishi anafufuka kutoka mautini, nchi ambayo ukienda hakuna kurudi, kupokea uadhimisho, kuona “uzao” wake, na kuishi siku nyingi (Isa. 53:10—12).
Chunguza kwa makini mafungu yafuatayo. Kila moja linaakisije ujumbe ule ule wa msingi kama Isaya 53?
Zab. 32:1, 2
Rum. 5:8
Gal. 2:16
Fil. 3:9
Ebr. 2:9
1 Pet. 2:24
Ikiwa mtu angekuuliza kufupisha kwa aya moja habari njema ya Isaya 52:13—53:12, ungeandika nini?
Post a Comment