mafunzo ya watu wazima leo 23
LESONI, MACHI 23
SOMO: WAMISHENARI NA VIONGOZI WA IBADA (ISA. 66:19—21)
Ni nini maana ya hao waliookoka uangamivu kwenda kuleta watu wa Mataifa kama sadaka kwa BWANA? Isa. 66:19, 20.
Mungu anawatuma hao waliookoka uangamivu wake waende miisho ya dunia, kwa watu wasiomjua Mungu, “nao watahubiri utukufu wangu katika mataifa” (Isa. 66:19). Hii ni kauli thabiti katika Agano la Kale kuhusu umishenari. Kwa maneno mengine, siyo tu kwamba watu watavutwa kuja kuwafuata Waebrania, ila baadhi ya Waebrania wataenda kwenye mataifa mengine na kuwafundisha kuhusu Mungu wa kweli —kauli itajwayo sana katika Agano Jipya. Japo kulikuwepo wamishonari wa Kiyahudi tangu kurudi toka uhamishoni hadi zama za Kristo (Mathayo 23:15), Wakristo wa awali walieneza injili kwa kazi na kwa kiwango kikubwa (Kol. 1:23).
Kama Waisraeli walivyoleta sadaka za nafaka kwa BWANA hekaluni, vivyo hivyo wamishenari watamletea BWANA sadaka. Lakini sadaka yao itakuwa “kuwaleta ndugu zao wote kutoka mataifa yote” (Isa. 66:20 ). Kama vile sadaka ya nafaka zilikuwa zawadi kwa Mungu ambazo hazikuchinjwa, waongofu walioletwa kwa BWANA watawasilishwa kwake kama “dhabihu iliyo hai” (linganisha na Rum. 12:1). Wazo kuwa watu wanaweza kutolewa kama aina fulani ya dhabihu kwa BWANA, zingatia uwekwaji wakfu wa Walawi hapo zamani “Naye Haruni atawasongeza Walawi mbele za Bwana wawe sadaka ya kutikiswa, kwa ajili ya wana wa Israeli, ili wawe wenye kufanya utumishi wa Bwana” (Hesabu 8:11).
Ni nini umuhimu wa ahadi ya Mungu ya "kuwatwaa baadhi kuwa makuhani na Walawi" (Isa. 66:21)?
Kauli “baadhi ya hao” katika aya ya 21 hurejea nyuma kwenye aya iliyotangulia iongeleayo “kuwaleta ndugu zao wote kutoka mataifa yote.” Hawa ni Mataifa, ambao baadhi Mungu atawachagua kama viongozi wa ibada, wakishirikiana na makuhani na Walawi. Haya ni mapinduzi makubwa. Zamani Mungu alikuwa ameruhusu tu ukoo wa Haruni kutumika kama makuhani na wenzao wa kabila la Lawi kuweza kuwasaidia. Watu wa Mataifa ukivuta fikra kwa upesi wasingeweza kuwa wazao wa ukoo wa Haruni au wa Walawi, ila Mungu anaidhinisha baadhi kutumika kwenye nyadhifa hizo, ambazo hapo awali zilikuwa haziruhusiwi hata kwa Wayahudi walio wengi.
Soma 1 Petro 2:9, 10. Je Petro anaandika kwa nani? Je ni nini anachosema? Anao ujumbe gani kwa kila mmoja wetu, kama washiriki wa “taifa takatifu” leo? Je tunatenda vyema zaidi kuliko taifa teule la awali (Kutoka 19:6)?
Post a Comment