amka na Bwana leo 23

KESHA LA ASUBUHI

JUMANNE, MACHI, 23, 2021
SOMO: TAZAMA MSAADA WAKE 

Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 

Waefeso 6:11 



Nyakati za hatari ziko mbele yetu. Dunia imepotoka, na itazidi katika upotovu. Lakini unaweza kuwa na tumaini kamilifu ndani ya Kristo. Licha ya vurugu, uhalifu, matumizi mabaya ya wanadamu ya fedha ambayo hawastahili, yupo Mungu ambaye ni mfalme juu ya ulimwengu. Sisi tu watoto wake, hatuko chini ya majaliwa ya kugeuka geuka. Tunayo, ndiyo, unayo, kama usomavyo maneno ya kutia moyo yaliosemwa na Kristo, ahadi takatifu itakayofanya upya chemchemi za matumaini. Unaweza kufurahi katika Mwokozi aliye hai. Yeye ni Bwana wetu aliyefufuka. Ahadi zake ni kwa wote watakaompokea. 



Masomo matakatifu katika Neno la Mungu hutuonesha kuwa mwanadamu kwa ukamilifu anapaswa kutendewa kwa heshima. Nguvu za akili, tamaa zenye nguvu, havipaswi kuvunjwa kama maadui, bali kuletwa chini ya utawala wa Kristo, vitumiwe katika kazi yake. Tukijivika kwa silaha zote, tunapaswa kufanya vita kwa ajili ya kweli na haki. Nguvu zetu zote zinapaswa kuwekwa wakfu kwa ajili ya hatima takatifu sana. 



Kristo alikuja kuwakomboa wanadamu. Anavutiwa na matendo yetu yote. Ana shauku ya kutuumba na kututengeneza katika mfanano wa kiungu. Kristo hatapumzika mpaka kila jambo litakapokuwa limeamuliwa. Nimeruhusiwa kuuona msaada wake, na upendo mkuu ambao ametupenda. Sina shaka yoyote kuhusu uongozi na maongozi yaliyopita ya majaliwa yake katika historia ya maisha yetu. 



Ninapaswa kuwa na hatia kama wana wa Israeli kama nisingejifunza masomo kutoka kwa mashutumu ambayo Mungu aliwapa. Kutotii ni lazima na kutaadhibiwa ikiwa wanaume na wanawake hawatageuka kutoka katika uasi na dhambi na kufanya sehemu ya udhaifu wao kuwa yenye nguvu kupitia kwa uangalizi wa kudumu. Giza litakuwa nuru kupitia utii ...... 



Kristo ametoa ujumbe, uliojaa baraka ya uweza wake. Alikuja kuwakomboa wanadamu, na ataendelea kutuma ujumbe baada ya ujumbe kuliokoa kundi lake kutoka katika madanganyo ya Shetani. Hatakoma kutuma jumbe zake mpaka ulimwengu uliokombolewa utakapopumzika. 

No comments