Askofu Niwemugizi .Mimi ndio nitamzika Magufuli,alisema

Chato. Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi amesema aliyekuwa Rais wa Tanzania marehemu, John Magufuli aliagiza arejeshewe hati yake ya kusafiria na alimtamkia  mara mbili kuwa kiongozi huyo wa kiroho ndiye atakayemzika.


Hati ya kusafiria ya Niwemugizi ilichukuliwa na Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 2017 pamoja na ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe na mkurugenzi wa taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze wote ikielezwa kuwa uraia wao ulikuwa ukichunguzwa.

Akizungumza leo Alhamisi Machi 25, 2021  katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato, Askofu Niwemugizi ambaye hakutaja muda maalum wa agizo la kurejeshewa hati hiyo, amesema Magufuli aliagiza idara ya uhamiaji kumrejeshea.

"Kwa kweli niwaambie mara mbili, Magufuli aliniambia, ‘wewe ni Askofu wangu utanizika. Mwaka ule 2015 akaniambia hivyo, mara ya pili akamwagiza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anirudishie passport akaniambia wewe ni Askofu wangu utanizika.”

No comments