amka na Bwana leo 3

*KESHA LA ASUBUHI* 

Jumatano 03/03/2021

*KUTAKA MAKUU KUNAKOKUBALIKA*

Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la BWANA mbele yako, nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili, nitamrehemu yeye nitakayemrehemu *Kutoka 33:19* 

▶️Katika wasilisho hili, Mungu anatamani kufundisha somo alolihitaji katika usafi wa tabia, utakatifu wa maisha. Ana shauku kuona ikifunuliwa ndani yao kuelekea kwa kila mmoja ishara za rehema na wema na ustahimilivu, kuwa watu wake waweze kuthibitisha kwamba “sheria ya BWANA ni kamilifu, huiburudisha nafsi” (Zaburi 19:7). Bwana yu tayari kujidhihirisha kwetu kama mioyo yetu inamtafuta na kumtumikia. Ni shauku yake muda wote kuwapatia baraka kubwa zaidi wale wanaomtumikia kwa moyo safi. Kristo atakuwa mwalimu wetu ikiwa tutaifungua mioyo yetu kwa maelekezo yake na kuitii sauti yake... 

▶️Ni mapenzi ya Bwana kuwa uweke mguso mpana kwa ajili ya mema. Je, umeamua kuwa Mkristo wa dhati? Basi, usishindwe wala kukatishwa tamaa. Hebu kazi yako iwe na mvuto unaoinua juu, ili uweze kuwa mtendakazi pamoja na Mungu. Bwana anatuhitaji sote tulitukuze jina lake. 

▶️Jana usiku mzigo mkubwa ulikuwa juu yangu kuhusiana na kazi kubwa inayotakiwa kufanywa. Ni kazi inayohitaji kutumia uwezo wote alionao mwanadamu. Je, hutatumia uwezo wako wote kwa namna ambayo itakuleta katika umoja mkamilifu na Yesu Kristo? Kama wazazi walimu tunapaswa kushirikiana na Mwalimu wa kiungu. Tunapaswa kufanya kazi kuwarejeshea wanaume na wanawake wazo la wajibu wa kimaadili lililopotea. Hebu kila mzazi sasa ashirikiane na mpango wa kiungu, na hivyo kuwa mtendakazi pamoja na Mungu. 

▶️Uwezo wetu wote anuwai ni wa Mungu. Ametununua kwa karama ya Mwanawe Wake wa pekee, na wale wenye wepesi wa kuhisi wajibu wao kwa Mungu watashirikiana na kusudi la kiungu. Wale wanaochukua majukumu katika kazi hii ya kutoa ujumbe wa malaika yule wa tatu kwa ulimwengu yawapasa waoneshe dhamira ya dhati katika kuipeleka mbele kazi ya Mungu. Moyo na nafsi na sauti vinapaswa kuwekwa wakfu kwake ili viweze kufikia kiwango cha juu sana cha ubora -mfano wa tabia ya Mungu. Kila kiungo, kila sifa ambayo Mungu ametupatia inapaswa kutumiwa kwa ajili ya kuwainua wanadamu wenzetu. Ikiwa tutafanya kwa ubora wetu, tukifanya kwa roho isiyo ya kibinafsi, Bwana atapokea utumishi wetu.

*MUNGU AKUBARIKI SANA*

No comments