amka na bwana leo 2

KESHA LA ASUBUHI

JUMANNE, MACHI, 2, 2021
SOMO: CHOCHEA KUPENDA 

Nalisema, Nitazitunza njia zangu, nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, maadamu mtu mbaya yupo mbele yangu. 

Zaburi 39:1. 



Watoto wangu, kesheni mkiomba, na iweni waangalifu zaidi na zaidi kwa habari ya maneno na matendo yenu. “Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni” (Mt. 26:41). Kumpatia adui hata manufaa kidogo ni sera iliyo dhaifu. Mwanangu, uwe muungwana, nawe utaimarisha mvuto wako juu ya wale unaofanya nao kazi. Kamwe usiseme bila subira. Hebu heshima yako kwako binafsi kama mwakilishi wa Kristo ikuzuie kuipa nafasi hasira. Ikiwa tunajiheshimu kwa kuivaa nira ya Kristo, tutaongeza mvuto wetu mara kumi zaidi. 



Asili ya mwanadamu itadumu kuwa asili ya mwadamu, lakini inaweza kupandishwa na kukuzwa hadhi kwa muungano na asili ya kiungu. Ni kwa kuishiriki asili ya kiungu kwamba wanaume na wanawake wataukwepa upotovu ulio katika dunia kupitia kwa tamaa. 



Kweli ni lazima itekelezwe ili kwamba ipate kuwa nguvu katika ulimwengu. Kweli inapokaa moyoni, uzoefu wa siku kwa siku ni ufunuo wa nguvu inayotawala ya neema ya Kristo. Kamwe msiiache kweli katika ua wa nje. Ruhusu Roho Mtakatifu aigonge kama muhuri katika moyo.... 



Mheshimuni Mungu na mali yake aliyoinunua. Iweni waangalifu sana na mienendo yenu, kwa kuwa ninyi ni wawakilishi wa Kristo. Chungeni maneno yenu kwa uangalifu, na fanyeni kazi kwa bidii kwa ajili ya kuwathibitisha na kuwaongoa wenye dhambi. Dumisheni kuinua mioyo kwa Mungu katika maombi. Wakati maneno yasio ya wema, yasio ya kweli yanasemwa kwenu, msishindwe kujitawala. Kumbukeni kwamba, “jawabu la upole huigeuza hasira” (Mit.15:1), na kwamba yeye aitawalaye roho yake ni mkuu kuliko mtu aitekaye mji.



Mkristo wa kweli ni muungwana. Wale waliojaa majivuno hudhani kwamba ni fursa yao kusema mambo mengi ambayo yangelipaswa kuachwa bila kusemwa. Maneno machache sana na matendo mengi ya wema yangewafanya nguvu kwa ajili ya mema. Mungu husema, "Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa" (Mt. 12:37). Maneno yetu yote na matendo, mema na mabaya, yanapita kwa kuchunguzwa mbele za Mungu. Ni fikra nzito kiasi gani! 



Neno la Mungu linatuonya ili tusichochee hasira sisi kwa sisi. Lakini kuna aina ya uchochezi unaohalalishwa. Paulo anaandika: ... "Tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kwa kazi nzuri" (Waebrania 10:24). 

No comments