amka na bwana leo 19

KESHA LA ASUBUHI

IJUMAA, MACHI, 19, 2021
SOMO: KUCHAGUA NA KUFANYA 

Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti; ili, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa. 

1 Petro 2:24. 



Ni kwa sababu Yeye [Kristo] aliibeba adhabu katika mwili wake mwenyewe msalabani ili mwanadamu awe na nafasi ya pili. Mwanadamu huyu anaweza, akitaka, kurudisha utii huu. Lakini, ikiwa atakataa kutii maagizo ya Mungu, ikiwa atayakataa maonyo na ujumbe anaoutuma Mungu, na badala yake kuchagua maneno ya uongo yanayosemwa na wale wanaotoa mwangwi wa maneno ya mdanganyifu, amekuwa mjinga kwa uhiari wake, na hukumu ya Mungu iko juu yake. Anachagua kutotii kwa kuwa utii unamaanisha kubeba msalaba na kujikana nafsi, na kumfuata Kristo katika njia ya utii. 



Moyo wa asili huegemea kuelekea kwenye anasa na kufurahisha nafsi na ni sera ya Shetani kutengeneza hili kwa wingi, ili waweze kujazwa na msisimko, pasipo kuwaachia wanaume na wanawake muda wa kuzingatia swali la, Nafsi yangu ina hali gani? Kupenda anasa kunavutia. Ikizoezwa katika hili, fikra huenda kwa haraka toka sehemu moja kwenda nyingine, ikidumu kutafuta maburudisho.... 



Uwezo wa kufurahia utajiri wa utukufu utaendelezwa kulingana na shauku tuliyonayo kwa ajili ya utajiri huu. Ni kwa namna gani utambuzi wa Mungu na mambo ya mbinguni utajengwa ikiwa si katika maisha haya? Ikiwa madai na masumbufu ya dunia yanaruhusiwa kushughulisha muda na usikivu wetu, nguvu zetu za kiroho hudhoofika na kufa kwa sababu hazitendewi kazi. Katika fikra iliyotolewa kwa mambo ya kidunia, sehemu zote zinazoweza kuruhusu nuru toka mbinguni kuingia zinafungwa. Neema ya Mungu ibadilishayo haiwezi kuhisiwa katika akili na tabia. Talanta zinazopaswa kutumika katika uchaji Mungu kweli kweli, zinadharauliwa na kutojaliwa. 



Ni kwa namna gani sasa mwitikio unaweza kufanywa wakati mwaliko unaposikiwa, "Njooni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari" (Luka 14:17)? Kwa namna gani inawezekana kwa kupokea sifa, “Vema, mtumwa mwema na mwaminifu,” wakati amekuwa mkaidi, asiye na shukrani, mwovu? Ametiisha akili yake katika kutojali maagizo ya Mungu ya wazi sana, kutokupenda mambo ya kidini. Anayapenda mambo ya dunia kuliko mambo ya mbinguni. 



Utii kwa maagizo ya Mungu utafanya majina yetu yaandikwe katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo, “Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo” (Waebrania 3:14).


No comments