WIZARA YA AFYA IMESEMA KILICHOTOKEA CHUNYA SIO MLIPUKO

• Wizara ya Afya imesema kilichotokea Chunya sio mlipuko - Kwa mujibu wa Mganga Mkuu Mbeya na Mganga Mkuu Chunya, kilichopo ni uwepo wa Wagonjwa waliowahi kuhudhuria katika vituo vya kutolea huduma tangu mwaka 2018 na kurudi nyuma ambao walibainika kuwa na homa mbalimbali zinazohusisha kuumwa tumbo na kutapika damu.

• Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya @wizara_afyatz imeendelea kueleza zaidi - Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dr. Doroth Gwajima ameagiza Timu ya Wataalamu husika wa Mkoa na Wilaya kuwasilisha kwake taarifa ya maandishi ifikapo kesho Jumapili saa sita mchana.

Waziri Gwajima amewaomba Wananchi kuwa Watulivu wakati Wizara ikifanya ufatiliaji wa kupata taarifa hiyo na kutoa ufafanuzi zaidi..... taarifa zilizotoka leo jioni zilimnukuu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chunya Ferister Kisandu akiongea baada ya kuwepo taarifa za Watu 15 kufariki na wengine zaidi ya 50 kuugua kisichofahamika.

• Tatizo hili halijaathiri Wilaya nzima bali Kata ya Ifumbo tu, Mtu anatapika damu.

• Tatizo hili halijaathiri Wilaya nzima bali Kata ya Ifumbo tu, Mtu anatapika damu akicheleweshwa Hospitali anafariki, tulituma Timu tukagundua wana vidonda vya tumbo, ugonjwa wa ini, Wanawake wachache Wanaume ndio wengi.

• Tumewapa Elimu ya Afya juu ya unywaji pombe, sigara na vitu vingine vikali, tumepeleka sample Mkoani ikiwemo maji kama wanahisi ni kemikali za Madini (dhahabu) tunasubiri utafiti wa Mkoa, idadi imekuwa kubwa lazima tuichukulie kwa ukubwa - Mganga Mkuu Chunya, Ferister Kisandu.
#BinagoUPDATES

No comments