PROF. MABULA MCHEMBE; KUWA NA TATIZO KATIKA MFUMO WA HEWA SIO KUUMWA CORONA

KUWA NA TATIZO KATIKA MFUMO WA HEWA SIO KUUMWA CORONA 

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Mabula Mchembe amewatoa hofu wananchi kwamba, kuwa na tatizo katika mfumo wa kupumua sio kuumwa ugonjwa wa Corona. 

Prof. Mchembe ametoa elimu hiyo leo wakati akiongea na Waandishi wa Habari, baada ya ziara yake katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa - Bugando na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou-Toure, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya nchini.
#BinagoUPDATES

No comments