Mafunzo ya watu wazima leo

LESONI, FEBRUARI 25

SOMO: MTUMISHI MWENYE HISIA NA MAUMIVU (ISA. 49: 1—12) 



Ni nani mtumishi wa Mungu katika Isaya 49:1—12?

Mungu anamwita na kumpa jina kabla hajazaliwa, anafanya kinywa chake kama upanga, naye atatukuzwa katika yeye. Mungu anamtumia mtumishi kulirudisha taifa la Israeli kwake, kuwa nuru ya wokovu kwa ulimwengu wote, kuwa agano, na kuwaachia huru wafungwa. Kuna kufanana kwingi kati ya maelezo haya na yale ya Isaya 42, tulipomtambua mtumishi kama Masihi. Agano Jipya humwona Yesu Kristo kama anayekidhi sifa za mtumishi, katika ujio wote: Mt. 1:21, Yohana 8:12, Yohana 9:5, Yohana 18 17:1—5, Uf. 1:16, Ufu. 2:16, Ufu. 19:15. 



Ikiwa huyu mtumishi ni Masihi, kwa nini Mungu anamwita “Israeli” hapa (Isa. 49:3)?

Awali tuligundua katika sehemu hii ya Isaya kuwa, mtumishi wa Mungu "Israeli/Yakobo" huwakilisha taifa. Lakini hapa jina “Israeli” (bila rejea inayofanana na “Yakobo”) kwa dhahiri huhusika na mtumishi mmoja, anayerejesha taifa kwa Mungu (Isa. 49:5). Mtumishi binafsi amekuwa mfano halisi au mwakilishi wa taifa ambalo kushindwa kwake kumeweka hatarini kutumia kwake jina “Israeli” (Isa. 48:1) 



Ni kipengele gani kipya kinaonekana hapa? Isa. 49:4, 7.

Haya ni maelezo ya awali ya ugumu unaohusika katika kazi ya mtumishi. Anaomboleza, “ ‘Nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida’ ” (Isa. 49:4), wazo linalorudiwa katika Danieli 9:26: “ ‘masihi atakatiliwa mbali naye atakuwa hana kitu.’ ” Bali anashikilia imani: “ ‘Lakini hakika hukumu yangu ina BWANA, na thawabu yangu ina Mungu wangu’ ” (Isa. 49:4). J. Alec Motyek anatoa wazo: “Hivyo, Isaya alitabiri kuhusu Mtumishi mwenye asili kamili ya mwanadamu, alijaribiwa sawasawa na sisi na kujithibitisha kuwa mwenye kuanzisha na kutimiza njia ya imani, halisi, imani binafsi ambayo bado yaweza kusema Mungu wangu wakati hakuna chochote zaidi kinachoonekana kuwa chenye kufaa.” —The Prophecy of 2 Isaiah: An Introduction and Commentary (Downers Grove, 3 Illinois: InterVarsity Press, 1993), uk. 387.



Isaya 49:7 inashtusha. Mtumishi anadharauliwa sana, anachukiwa na mataifa, mtumishi wa watawalao,” lakini mwishoni Bwana anamwambia: " 'Wafalme wataona watasimama,; wakuu nao watasujudu, kwa sababu ya BWANA aliye mwaminifu, Mtakatifu wa Israeli aliyekuchagua.’ ” 



Tazama nyuma katika huduma ya Kristo. Kwa haraka mpaka mwisho, je, hakuwa na sababu za kukatishwa tamaa? Japo, alibakia mwaminifu, licha ya mwonekano wa nje. Ni somo gani kwa ajili yetu kufanya vivyo hivyo licha ya mwonekano wa njema
Share ⏬

No comments