amka na Bwana leo 25
KESHA LA ASUBUHI
ALHAMISI, FEBRUARI, 25, 2021
SOMO: AMINI NA KUTII
BWANA asema hivi; amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake.... Amebarikiwa mtu yule amtegemeaye BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake
Yeremia 17:5—7.
Kama Wayahudi katika siku za Kristo, wengi leo husikia na kuamini, lakini hawako tayari kupiga hatua katika jukwaa la utii, na kupokea kweli kama ilivyo katika Yesu. Wanaogopa kupoteza fursa za kidunia. Mioyo yao huikubali kweli lakini kutii humaanisha kubeba msalaba wa kujikana nafsi na kutoa kafara, na kuacha kumtumainia mwanadamu na kumfanya mwanadamu kuwa kinga yao, na kugeuka mbali toka katika msalaba. Wangeweza kukaa miguuni pa Yesu, wakijifunza kwake kila siku Yeye ambaye kumjua sawasawa ni uzima wa milele, lakini hawako tayari.
Kila mmoja aliyeokolewa ni sharti asalimishe mipango yake mwenyewe, mipango yake ya kutaka makuu, inayomaanisha kujitukuza nafsi, na kufuata pale Kristo anapotuelekeza. Utambuzi sharti utolewe kwa Kristo, kwa ajili ya kuoshwa na kutakaswa, na kusafishwa. Hili litafanyika mara zote ikiwa upokeaji sahihi hutolewa kwa mafundisho ya Bwana Yesu. Ni vigumu kwa nafsi kufa kila siku, hata wakati ambapo kisa cha ajabu cha neema ya Mungu hutolewa na utajiri wa pendo lake, ambacho Anakifunua kwa manufaa ya nafsi.
Ni kwa kiasi gani tunahitaji kumfahamu kwa karibu zaidi Bwana Yesu. Tunahitaji kuingia katika nia yake na kulibeba kusudi lake, tukisema kwa moyo wote, “Bwana, unataka nifanye nini?” Ni shauku kiasi gani niliyo nayo kuona makanisa yetu yakiwa katika hali tofauti na hali yaliyonayo sasa —yakimhuzunisha Roho siku kwa siku kwa maisha vuguvugu ya kidini, maisha yasiyo baridi wala moto. Kristo anasema, “Ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu” (Ufunuo 3:15, 16).
Ni kwa kiasi Kristo angeheshimiwa na kutukuzwa sana mbele ya wale wasio na dini, wanaume na wanawake wenye kuifuata dunia ikiwa wafuasi wake wangekuwa kile wanachodai kuwa —Wakristo wa kweli, upendo wa Kristo ukiwabidisha kumfanya ajulikane mbele ya ulimwengu uliojaa ibada ya sanamu, wakionesha alama zinazotofautisha kati ya wale wanaomtumikia Mungu na wale wasiomtumikia.... Tunapaswa kuwaambia wengi juu ya upendo wa Kristo, na ili kufanya hili, ni sharti tujue kwa uzoefu maana ya kuwa na pendo hili moyoni. Wote watapata fursa nyingi ikiwa wataboresha fursa zinazowajia.
Post a Comment