mafunzo ya watu wazima leo 7

LESONI, FEBRUARI 7

SOMO: MASHARTI YALIYOUNGANISHWA (ISA. 36:1)



Kitu gani kiliipata Yuda? 2 Wafalme 18:13, 2 Nyakati. 32:1, Isa. 36:1.



Wakati Ahazi asiye na imani alipokufa na mwanawe mwaminifu Hezekia akatawala badala yake, Hezekia alirithi ufalme uliopoteza uhuru mkamilifu. Kwa kununua msaada wa Ashuru dhidi ya muungano wa Shamu na Israeli ya kaskazini, Yuda alilazimika kuendelea kulipia "gharama ya ulinzi" kwa njia ya kulipa kodi kwa Waashuru (tazama 2 Nyakati 28:16—21). 



Wakati mfalme wa Ashuru Sargoni II alipokufa kwenye uwanja wa mapambano na nafasi yake kuchukuliwa na Senakeribu katika mwaka wa 705 K.K., Ashuru ilionekana kuwa dhaifu. Ushahidi kutoka Ashuru na mafungu ya Biblia hudhihirisha kwamba Hezekia alitumia hii fursa kuasi (tazama 2 Wafalme 18:7), akichukua uamuzi wa shari kama kiongozi mwanzilishi wa uasi dhidi ya Ashuru miongoni mwa mataifa madogo katika eneo lake. 



Kwa bahati mbaya kwake, hakukadiria kwa usahihi uwezo wa Ashuru kurejesha uimara wake. Katika mwaka 701 K.K., wakati Senakeribu alipoyashinda maeneo mengine ya himaya yake, ghafla alivamia Shamu-Palestina kwa nguvu ya kuharibu na kuleta uharibifu mkubwa kwa Yuda. 



Hezekia alijiandaaje kwa makabiliano na Ashuru? 2 Nyakati 32:1—8

Hezekia alipoona kwamba Senakeribu amedhamiria kuichukua Yerusalemu, mji mkuu, alifanya maandalizi makubwa kwa ajili ya makabiliano na Ashuru. Aliimarisha ulinzi wake, alitayarisha na kuliandaa jeshi lake, na kuboresha sana upatikanaji wa maji mjini Yerusalemu (tazama pia 2 Wafalme 20:20, 2 Nyakati 32:30). Mfereji wa maji wenye kusifika wa Siloamu, uliowekewa ukumbusho kwa maandishi yanayoeleza jinsi ulivyojengwa, karibu kwa hakika ilikuwa katika wakati wa maandalizi ya Hezekia kwa ajili ya uwezekano wa kuzingirwa. 



Kama vile jeshi na muundo wa uongozi vilivyo muhimu, Hezekia aliandaa uongozi wa kiroho alipokuwa akitafuta kuongeza ari ya watu wake katika wakati huu wa kutisha. “Lakini mfalme wa Yuda alikuwa amedhamiria kufanya sehemu katika kujiandaa kumpinga adui; na, baada ya kukamilisha yote ambayo maarifa ya mwanadamu yanaweza kufanya, aliyakusanya majeshi yake naye aliwasihi wawe na moyo mkuu.” —Ellen G. White, Prophets and Kings, uk. 351.



Ikiwa Hezekia alimtumaini sana Bwana, kwa nini aliweka jitihada kubwa yeye mwenyewe? Je, kazi yake ilitangua imani yake? Tazama Wafilipi 2:12, 13 katika kushirikiana na Mungu, ambaye hutoa uwezo ambao unafaa kwa hakika.


No comments