mafunzo ya watu wazima leo 20
LESONI, FEBRUARI 20
SOMO: KUHUDUMU NA KUOKOA
SABATO MCHANA
Somo la Juma Hili: Isa. 41, Isa. 42:1—7, Isa. 44:26—45:6, Isa. 49:1—12.
Fungu la Kukariri: " 'Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye, mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye, nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu' " Isaya 42:1
Wengi wanahisi kwamba ingekuwa fadhila kubwa kutembelea mandhari za maisha ya Kristo akiwa duniani, kutembea alipokanyaga, kutazama ziwa ambako alikuwa akipenda kufundisha kando yake, na vilima na mabonde ambapo macho yake mara nyingi yalitazama. Lakini hatuhitaji kwenda Nazareti, Kapernaumu au Bethania, ili kutembea katika nyayo za Yesu. Tutazikuta nyayo zake kando ya kitanda cha mgonjwa, katika vibanda vya maskini, kwenye vichochoro vya mji mkubwa vilivyojaa watu, na popote pale palipo na mioyo ya wanadamu yenye kuhitaji faraja. Kwa kufanya kama alivyofanya Yesu alipokuwa duniani, tutatembea katika nyayo zake.” —Ellen G. White, The Desire of Ages, uk. 12 640.
Isaya alizungumza kuhusu mtumishi wa Bwana akiwa na utume ule ule wa rehema: "mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; ... kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa" (Isa. 42:3, 7). Hebu tumtazame huyu Mtumishi. Yeye ni nani, Naye anatimiza nini?
Jifunze somo la juma hili ukijiandaa kwa ajili ya Sabato ya Februari 27.
Post a Comment