mafunzo ya watu wazima leo 16
LESONI, FEBRUARI 16
SOMO: CHIMBUKO LA UINJILISTI (ISAYA 40:9—11)
Ni tukio la namna gani linaelezewa katika 40:9—11
Baadaye katika Isaya anatokea mjumbe mwanamume mwenye habari njema kwa Yerusalemu (Isa. 41:27, Isa. 52:7). Lakini katika Isaya 40:9 mjumbe kutangaza " 'Tazameni, Mungu wenu!' " kutoka mlimani ni wa kike, ukweli unaotolewa katika Kiebrania.
Katika Zaburi 68, Daudi anamsifu Mungu kwa kuwa “huwakalisha wapweke nyumbani; huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa” (Zab. 68:6). Japo hapa maneno haya hutumika kwa Waliotoka katika utumwa wa Misri, Isaya anatumia wazo lile lile kurejelea utangazwaji wa “Kutoka” wa pili: kurejea kutoka utumwa wa Babeli.
Wakati uo huo, Agano Jipya hutumia Isaya 40:3—5 kwa Yohana Mbatizaji, aliyetengeneza njia kwa ajili ya Kristo, Neno la milele aliyefanyika uwepo wa Bwana katika mwili miongoni mwa watu Wake (Yohana 1:14).
Hata mapema kabla ya Yohana, wengine walitangaza habari njema ya kuja kwake. miongoni mwa wa kwanza wa hawa walikuwa wazee Simioni na Ana, waliokutana na Yesu alipowekwa wakfu hekaluni (Luka 2:25—38). Kama vile wajumbe wa Isaya, walikuwa wa kiume na wa kike. Simioni alikuwa anatazamia mfariji/faraja ya Israeli katika muundo wa Masihi (Luka 2:25, 26)
Katika mwanga wa unabii wa Isaya, haitokei kwa nasibu kwamba Ana, nabii wa kike, alikuwa wa kwanza kabisa kutangaza hadharani katika mlima wa hekalu kwa watu wa Yerusalemu kwamba alikuwa amekuja: “Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake” (Luka 2:38).
Hili lilikuwa chimbuko la uinjilisti wa Kikristo kama tuujuavyo: utangazwaji wa injili, habari njema, kwamba Yesu Kristo amekuja kuleta wokovu. Baadaye, Kristo alikabidhi kwa mwanamke mwingine, Mariamu Magdalena, habari za kwanza za ufufuo wake wa kishujaa (Yohana 20:17, 18), uliotoa uhakikisho kwamba utume wake wa injili kwa sayari Dunia ulikuwa umekamilika. Mwili ni kama majani, lakini Neno la Mungu aliyefanyika mwili ni la milele (tazama Isa. 40:6—8)
Tazama 40:11. Ni picha gani inawasilishwa hapa? Andika kwa ajili yako aya moja juu ya namna wewe, binafsi, umepitia uzoefu wa kuchungwa na Bwana. Kwa nini ni vizuri kukumbuka akilini mwako jinsi Bwana alivyokuongoza?
Post a Comment