HAJI MANARA AKIWA KWENYE PRESS NA SALAMA JABIR, NILIZALIWA AMSTERDAM ✍

"Mimi nimezaliwa Amsterdam, Uholanzi. Nimezaliwa wakatai baba yangu akiwa anacheza mpira sana wakati huo. Mama yangu ni mtoto wa Mwenyekiti wa Simba wakati huo" - HajiManara

"Ndoa ya mzee wangu na mama ilikuwa kubwa sana wakati huo ni sawa sawa na sasa hivi Chama amuoe mtoto wa Dkt. Msolla wa Yanga" 

"Siku hiyo ya ndoa yao, wakinamama upande wa baba walivaa khanga za Pele na Santos kwa sababu walitaka kuialika Santos Tanzania na upande wa mama walivaa khanga za 'Simba bingwa 1973" 

"Baba yangu hakuwahi kunichagulia timu, vitu nilivyokuwa napenda ni vyekundu na wakati huo anacheza Ulaya ananiletea zawadi ya vitu vya rangi hiyo. Kuna siku nililetewa viatu vya njano nikamuita mtoto wa jirani nikampa"

"Mzee wangu kipindi hicho anatoka Uholanzi alikuwa haswali, siku moja nikawakusanya Masheikh na wenyewe walidhani kuna ubwabwa, kufika nyumbani nikawaambia baba yangu huyu haswali lakini leo yeye ndiye ananisihi kuswali" 

"Mimi naamini jina langu na baraka ninazopata ni kutokana na maneno na matusi ya watu hao. Pesa ninazopata na mikataba ninayopata ni kutokana na matusi yao, mimi sijawahi kuitukana Yanga na siku nikiitukana watanistaki"

"Mimi sitaki pesa, sitaki kuwa Mo Dewji wala Bakhresa ila mimi nataka sifa tu niwe mkubwa ili hata nikija kuondoka watu wasema kuna huyu mtu alikuwepo hapa nchini na alifanya hivi"

"Mimi ni mtu namba moja ambaye siwezi kutoa siri za klabu yangu, mke wangu hawezi kujua wala dereva wangu. Lakini wakina Ghalib na Eng. Hersi ni rafiki zangu na watu wanaokasirika mimi kukaa nao nawaambia siachi" 

"Ninaloamini kwenye moyo wangu ni kuwa Mo ataweka pesa, kuhusu lini ataweka ni mpaka hapo mambo yatakapokaa sawa. Kipindi cha mgogoro wa Mo na Kigwangalla nilikaa pembeni natizama tu na baada ya kutulia nilitoa ujumbe mzuri"- HajiManara

"Kabla ya hii ndoa yangu kuliwahi kuwa na mgogoro kwenye familia kiasi kwamba nikawa nashindwa kuubeba kwenye moyo wangu, nitakuja kuzungumza siku moja. Ilifikia kipindi nilitamani niwaache watoto kwa mama nikaishi huko nje"- HajiManara 
#BinagoUPDATES

No comments