AMRI KIEMBA; LUIS MIQUISSONE NDIO MCHEZAJI HATARI ZAIDI KATIKA KIKOSI CHA SIMBA
Kwa Mujibu wa Amri Kiemba anasema, Jose Luis Miquissone ndiye mchezaji hatari zaidi katika kikosi Cha SIMBA kuliko mchezaji yoyote yule
Kwanini?
Kiemba anasema, Simba bado hawajaweza kumtumia Miquissone katika eneo lake sahihi, bali wanampa maeneo magumu zaidi.
Kikawaida uwanja una maeneo matatu, yaani kuna eneo la ushambuliaji, eneo la ulinzi na eneo la kiungo kwamaana ya Malengo.
Kwa mfumo wa SIMBA, Luis Miquissone anapewa majukumu mawili, kwanza kusaidi kwenye kukaba Kisha kushambulia ila Kama angekuwa free kucheza eneo la ushambuliaji pekee kama ilivyo kwa Chama, basi huyu angekuwa anafunga kila siku.
Amri Kiemba anaamini majukumu ya Chama ni machache sana hasa kushambulia peke yake kuliko anavyofanya Luis Miquissone.
Vipi unakubaliana na Kiemba kwa asilimia ngapi katika hili?
#BinagoUPDATES
Post a Comment