Unabii sehemu ya 1,siku za mwisho zimefika
Yatupasa kuyajua na kufunuliwa haya
BWANA atukuzwe🙏. Yeye ambaye amejiweka wakfu kwaajili yetu milele bado anatulinda🙏🏻.
Rafiki zangu wasomaji! Leo nawakaribisha katika somo makini kabisa ambalo ni la #UNABII muhimu kabisa ambao tunapaswa kuufahamu Wanadamu wote hasa Waadventista WASABATO wa leo. Wewe kama ni mwadventista MSABATO makini na ambaye upo safarini kuelekea Mbinguni kwa BABA MTAKATIFU MUNGU WETU, lazima uzijuwe ishara za #UNABII huu ambao unazidi kutimia kwa kasi ajabu. Sehemu kubwa ya unabii huu umetimia, bado sehemu ndogo tu nayo inazidi kutengeneza njia ya utimilivu kwa kasi ajabu.
Leo naangazia kitabu cha #DANIELI SURA YA 7:1-28
#DANIELI 7:1-28
........................................................................................................................................................................
Danieli 7:1-3
Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza mfalme wa babeli, Danieli aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake, basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo, Danieli akanena akasema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku, na tazama hizo pepo nne za Mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa. Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali.
Danieli sura ya 7 na danieli sura ya 2 zina vitu vinavyofanana. Katika danieli 2 tunamuona Mfalme nebukadreza anaota ndoto ya sanamu kubwa yenye madini ya aina nne ambayo yaliwakilisha falme nne au tawala nne tofauti, katika danieli sura ya 7 Danieli anaota ndoto ya wanyama wakubwa wanne tofauti, wanyama hao wakiwakilisha falme 4 au tawala 4 tofauti zitakazotawala dunia. Kwa hiyo danieli 7 na danieli 2 yapo mambo mengi ambayo ni kitu kimoja. Ila danieli sura ya saba inayo maelezo ya ziada.
VITU VYA KUANGALIA KATIKA SURA YA 7 YA DANIELI ILI TUWEZE KUPATA MWANGA WA UNABII HUU WA DANIELI NI:👇🏻👇🏻
Ni nini maana ya👇🏻👇🏻👇🏻
1. UPEPO
2. BAHARI/MAJI
3. MNYAMA/WANYAMA
UFAFANUZI NI HUU KUPITIA BIBLIA YENYEWE👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻
UPEPO = Ni machafuko ya kisiasa au ghasia.
Yeremia 25:32
BAHARI/MAJI = Ni watu/Jamii ya watu wengi/
Mataifa na Lugha.
Isaya 57:20. Ufunuo 17:15
MNYAMA/WANYAMA = Ni ufalme/wafalme/
Serikali.
Danieli 7:17
Mnyama wa kwanza alikuwa ni SIMBA✓
.....................................................................
Danieli 7:4
Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya Tai, nikatazama hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi , akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu , naye akapewa moyo wa kibinadamu.
👉🏻Simba ni mnyama wa kwanza katika Danieli 7:4.
👉🏻Simba anawakilisha ufalme wa Babeli
👉🏻Mabawa ya Tai huonyesha uhodari na wepesi wake kivita. Habakuki 1:6-8, Yeremia 48:40. Torati 28:49-50
👉🏻Simba ni sawa na kichwa cha dhahabu cha sanamu aliyoota nebukadreza. Daniel 2:38
👉🏻Ufalme wa babeli ulianza kutawala dunia mwaka 605-539BC
Daniel 5:25-28.
Nebukadreza alianza kutawala dunia mwaka wa 605 hadi 539bc .
Baba yake nebukadneza Nabopolasa katika mwaka wa 612bc aliuangamiza mji wa ninawi , na kuvunja kabisa nguvu za utawala mkuu wa ashuru , na hivyo kuweka misingi ya babeli kutawala dunia.
Mtoto wake aitwaye nebukadreza akamalizia kazi ya babake. Nebukadreza akamshambulia farao Neko mfalme wa misri karibu na karkemishi kando ya mto frati mnamo mwaka 605bc . Nebukadreza akalishambulia Taifa la Yuda na badaye kuangamiza mji wa Yerusalemi mwaka 586bc. 2Waf 25:8-15.
Baada ya hapo Babeli ikawa mtawala mkuu wa dunia. Mwaka 605BC -539BC
Utawala huu ulikuwa ni wa kifahari, lakini uliojaa kiburi na ibada ya sanamu. Wababeli walikuwa waabudu miungu. Babeli ya zamani iliangamia sababu ya kutomheshimu MUNGU aliye juu.
Kwahiyo mnyama Simba aliwakilisha utawala wa Babeli ile ya zamani.
Post a Comment