UJIO WA MESUT OZIL FENERBAHCE UNAWEZA KUMFANYA SAMATTA ANG'AE ZAIDI
HABARI njema kwa mashabiki wa Fenerbahce ya Uturuki na wafuasi wa nahodha wa Taifa Stars, ni Mbwana Samatta ‘Samagoal’ ni kutua kwenye klabu hiyo kwa supastaa wa Kijerumani, Mesut Ozil, ambaye alifanya makubwa kwenye Ligi ya Ujerumani (Bundesliga), Hispania (LaLiga) na England (EPL).
Ipo imani kwa Watanzania Samatta anaweza kung’ara zaidi Ozil akitua Fenerbahce kutokana na uwezo alionao kiungo huyo katika kutengeneza nafasi za mwisho kwani kote alipopita alikuwa mfalme wa asisti.
Tujikumbushe kidogo; wakati akiwa Ujerumani na klabu ya Werder Bremen msimu wa 2009/10, Ozil alitwaa tuzo ya kuwa mchezaji aliyetengeneza mabao mengi zaidi, 17, alimzidi Zvjezdan Misimovic wa VfL Wolfsburg kwa asisti mbili. Ndani ya msimu huo wa Ligi Kuu Ujerumani akawa kiungo bora wa msimu.
Ndani ya mwaka huo, 2010 alienda Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia akiwa na Ujerumani ambako alitwaa tena tuzo ya mtoaji asisti bora, akitoa tatu. Ozil alionyesha ni balaa kwenye upigaji pasi za mwisho hata akiwa Hispania na Real Madrid na alitwa tuzo hiyo, 2010/11, 2011/12, 2012/13.
#BinagoUPDATES
Post a Comment