NCHINI KENYA POLISI AMPIGA RISASI MWALIMU

KENYA; POLISI AMPIGA RISASI MWALIMU

Maafisa wa polisi wa Kaunti ya Turkana nchini Kenya wamemkamata mwenzao baada ya kudaiwa kumuua mwalimu wa kike kwa kumpiga risasi.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, Konstebo Kibichiy ambaye alikuwa akihudumu katika kituo cha polisi cha Kakong alitekeleza kitendo hicho jana Jumanne, Januari 12 akiwa katika soko la Kakong. 

Afisa huyo inasemekana alikunywa pombe kwenye klabu moja inayomilikiwa na mwalimu huyo katika soko hilo. 

Inadaiwa kuwa ugomvi ulizuka muda mchache baadaye ambapo, Susan Nasiru Emure ambaye ni mwalimu wa shule ya upili alimtaka Afisa huyo kulipia bia hizo Ksh 500(Sh 10,000).

Katika harakati za kuvutuna na kurushiana matusi, mwalimu huyo anasemekana kumpiga Wilfred jiwe kichwani na kuanza kuvuja damu.

Akiwa mwenye hasira, Afisa huyo aliondoka hadi kutuoni na kuchukua bunduki aina ya G3, na kumfuata mwalimu huyo aliyekuwa tayari amefika nyumbani kwake na kumfyatulia risasi kadhaa hadi kufariki paop hapo.

Maafisa wa upelelezi waliofika eneo la tukio walithibitisha kuwa marehemu alikuwa na majeraha ya risasi.

Mshukiwa anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Lodwar huku uchunguzi kuhusiana na kisa hicho ukiendelea.
#BinagoUPDATES

No comments