mafunzo ya watu wazima leo 30 mchana
LESONI, JANUARI 30
SOMO: KUJIFANYA MUNGU
SABATO MCHANA
Somo la Juma Hili: Isaya 13, Isa. 13:2—22, Isaya 14, Isaya 24—27.
Fungu la Kukariri: "Tazama huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye Bwana tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake" (Isaya 25:9).
Baada ya mchungaji kutoa hubiri lenye mguso juu ya kiburi, mwanamke aliyekuwa amesikiliza hubiri alimsubiri mchungaji akamwambia kuwa alikuwa akisumbuka akilini, na kuwa alitaka kuungama dhambi kubwa. Mchungaji alimwuliza dhambi ile ilikuwa ni nini. “Mwanamke alijibu, ‘Dhambi ya kiburi, kwani nilikaa kwa saa moja mbele ya kioo changu siku kadhaa zilizopita nikihusudu uzuri wangu.’ —" 'Oo' mchungaji aliitikia, 'hiyo haikuwa dhambi ya kiburi —hiyo ilikuwa dhambi ya fikra!' " —C. E. Macartney, compiled by Paul Lee Tan, uk. 1100.
Tangu dhambi ilipozaliwa katika moyo wa malaika mkuu, kiburi hakijali mipaka ya uhalisia (kwa malaika au wanadamu). Tatizo hili linaonekana kuwa kubwa zaidi kwa wale wanaokuwa na kiburi cha kiroho, tabia ya kusikitisha miongoni mwa viumbe walioharibika sana kiasi ambacho wokovu wao unaweza kupatikana tu kwa njia ya kazi za mwingine kwa niaba yao.
Juma hili, miongoni mwa mambo mengine, tutaangalia chanzo cha kiburi na kujiinua, dhambi mbili ambazo kwa kweli ndizo dhambi halisi.
Jifunze somo la juma hili ukijiandaa kwa ajili ya Sabato ya Februari 6.
Post a Comment