unabii sehemu ya 7,kubadilisha majira na sheria

PEMBE NDOGO(UPAPA) ILIBADILI MAJIRA NA SHERIA.

UNABII:sehemu ya saba.

Danieli 7:25
👉🏻Naye ataazimu kubadili majira na sheria.

Kwa kiburi kabisa upapa ulikusudia kubadilisha amri za MUNGU na pia kubadili majira. Hesabu ya mbingu katika majira inafahamika kama hivi👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻
Siku huanza jioni jua linapozama na kuisha jioni jua linapizama, ikiwa na masaa ishirini na nne. Jioni inawakilisha masaa kumi na mbili ya giza, na asubuhi inawakilisha masaa kumi na mbili ya Nuru. Huu ni utaratibu ambao MUNGU aliuweka ili Wanadamu tuutumie.

Upapa ukabadili, ukasema siku inaanza saa sita kamili usiku wa manane na siku inaisha saa sita usiku wa manane. Na hii imekuwa desturi ya dunia nzima leo, hadi Waadventista Wasabato wengi wanafuata mtindo huu na kuupa upapa heshima bila kujuwa hili ni kosa.

Mwezi una siku 30 tu kwa ratiba ya Mbinguni , mwaka una miezi 12. Mwaka una siku 360 tu.

Upapa ukabadili, mwaka una siku 365 hadi 366, miezi ikaongezwa siku, 1 hivyo unakuta mwezi una siku 31 na mwezi wa pili ukapunguziwa siku ukapewa siku 28. Haya ni mabadiliko yaliyofanywa na taasisi ya upapa.

Upapa ukabadili AMRI za MUNGU . Amri ya pili inayokataza kujifanyia sanamu za kuchonga na kuziabudu, imeondolewa katika amri za kanisa la Roman Catholic .Amri ya SABATO ya BWANA imeondolewa na ikapewa jumapili kuwa ndiyo sabato. Amri ya 10 imegawanywa kuwa mbili. Na hii ndiyo maana ukiwauliza waromani katoliki swali, #USIZINI ni amri ya ngapi?? Wakatoliki watakuambia ni amri ya sita🤣🤣🤣 wakati kwa mujibu wa biblia hiyo ni Amri ya saba. Yani hawa watoto wa Mungu walioko huko wamechanganywa kimafundisho na hata biblia hawasomi kabisa, na hata wakisoma hawajui wasomacho maana huko hakuna mwalimu.

Hebu tumsikilize huyu kiongozi wa kanisa katoliki asemavyo:👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

PRIEST BRADY, katika hotuba yake iliyoripotiwa kule Elizabeth, New Jersey, The News,
      March 18, 1903.

👉🏻Ni vema kuwakumbusha wapresbiteriani, wamethodisti, na wakristo wengine wote kwamba, BIBLIA haiwaungi mkono popote katika utunzaji wa jumapili. Jumapili ni pando la kanisa katoliki la kirumi, na wale wanaoitunza siku hiyo wanatunza amri ya kanisa katoliki. Kuhusiana na badiliko kutoka utunzaji wa SABATO ya kiyahudi kwenda jumapili ya kikristo , ninataka kuvuta usikivu wenu katika ukweli huu.👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

1. 👉🏻Kwamba waprotestanti wanaokubali biblia kama msingi wa imani yao na dini, sharti kwa hali zote warejee katika utunzaji wa SABATO (jumamosi). Ukweli kwamba hawafanyi hivyo, huwafanya kuwa kituko machoni mwa kila mtu mwenye kutafakari sawasawa.🤔🤔

2. 👉🏻Sisi wakatoliki hatukubaliani na biblia pekee kama msingi wa imani. Mbali na biblia tunayo mapokeo ya kanisa kama msingi wa kutuongoza. Kanisa katoliki la kirumi lililopewa mamlaka na kristo kufundisha na kuelekeza mwanadamu maishani lina haki kubadilisha sheria za musa za agano la kale na hivyo sisi wakatoliki tunakubali badiliko la sabato kwenda jumapili.
👉🏻Ndiyo tunasema wazi wazi kuwa kanisa ndilo lilifanya badiliko hili, lilitunga sheria hii, kama lilivyotunga sheria nyinginezo nyingi, kwa mfano👇🏻👇🏻👇🏻

Ijumaa kuu ya kujinyima
Mapadre kutooa
Sheria kuhusiana na ndoa za jinsia moja au mchanganyiko, kurekebisha ndoa za kikatoliki na maelfu kadhaa ya sheria.

Huyu ni miongini mwa viongozi wakubwa wa kikatoliki ambaye anatoa ushuhuda huu👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻

Hebu tumwangalie na huyu mwandishi pia👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

PETER KRAEMER, 
CATHOLIC CHURCH, EXTENSION MAGAZINE, 
USA (1975) CHICAGO, ILLINOIS ,
UNDER THE BLESSING OF
POPE PIUS XI

👉🏻Mara nyingi ni kitu cha kuchekesha, kuyaona makanisa ya kiprotestanti, katika mimbari na hata mabunge, yakitetea utunzaji wa jumapili ambayo haiungwi mkono na BIBLIA .

Mpendwa msomaji, BWANA hajawahi kukosea, na anao watu waaminifu duniani ambao huwatumia kutunza ushahidi ili mwenye kuamini aokolewe na asiyeamini ahukumiwe.

Upapa ndio uliohusika na mabadiliko ya sheria za MUNGU na hata majira, wao wenyewe wanakubali hilo kabisa bila kupindisha ukweli.

Mpendwa msomaji, nakualika katika kanisa la kweli la MUNGU Muumbaji , uungane na ndugu zako, wasafiri katika njia ya kweli, wale wazishikao AMRI za MUNGU na imani ya YESU , ikiwemo SABATO Takatifu ambayo inamtambulisha MUNGU kuwa ndiye Muumbaji wetu.

BWANA awabariki na awasaidie kuijuwa hii kweli muhimu.

YESU anakuja,
Bado kitambo kidogo
Yeye ajaye atakuja
Na wala hatakawia.

BWANA awabariki mno. Endelea kufatilia ukurasa huu/hii page nawe hutojuta.🙏🏻

No comments