mafunzo ya watu wazima leo 16 mchana
LESONI, JANUARI 16
SOMO: NJIA YA TABU
SABATO MCHANA
Somo la Juma Hili: Isa. 7:14—16 Isa. 7:17—25, Isa. 8:1—10 Isa. 8:11—15, Isa. 8:16—22
Fungu la Kukariri: "Nami nitamngojea Bwana, awafichaye uso wake nyumba ya Yakobo, nami nitamtazamia" (Isaya 8:17).
Katika jengo lililokuwa likiungua moto eneo la Harlem Jijini New York, binti asiyeona alionekana katika dirisha la ghorofa ya nne. Askari wa jeshi la zima moto walikuwa na wakati mgumu. Hawakuwa na ngazi ambayo ingetosha kuwasaidia kumwokoa na hawakuweza kumshawishi aruke na kuangukia kwenye wavu, ambao, hata hivyo asingeweza kuuona.
"Hatimaye Baba yake alifika na kupiga kelele kwa kutumia pembe ya dume la ng’ombe akisema kulikuwa na wavu na alipaswa kuruka akimwamurisha kufanya hivyo. Binti aliruka na alikuwa mtulivu kabisa kiasi kwamba hakuvunjika mfupa wala kupata mchubuko wo wote kwa kuruka kutoka ghorofa ya nne. Kwa kuwa alimwamini baba yake kikamilifu, aliposikia sauti ya baba yake alifanya kile ambacho baba yake alimwagiza kukifanya" —Edited by Michael P. Green, 1500 Illustrations for Biblical Preaching, uk. 135.
Hali kadhalika, Mungu alitoa ushahidi wenye nguvu kuwa alikuwa na nia njema kwa ajili ya watoto Wake, lakini walikataa njia ya maongezi ya upole aliyotumia mwanzoni; hivyo, ilimpasa kuzungumza kwa ngurumo na mafuriko badala yake.
Ni masomo gani tunaweza kujifunza leo kutokana na makosa yao?
Jifunze somo la juma hili ukijiandaa kwa ajili ya Sabato ya January
Post a Comment