Mafunzo ya watu wazima leo 11

LESONI, JANUARI 11

SOMO: JARIBIO LA KUINGILIA KATI (ISA. 7:3—9)



Wakati Ahazi alipokuwa akifikiria maamuzi ya kisiasa ambayo ilimpasa kuyafanya kuhusiana na tishio la Israeli na Shamu, Mungu alijua mambo ambayo Ahazi hakuyajua. Kwa upande mmoja, ni Mungu aliyekuwa ameruhusu matatizo yampate ili kum—nidhamisha na kumfanya ajitambue (2 Nya. 28:5, 19). Zaidi ya hapo, ingawa kutafuta msaada kwa Tiglath-pileser kulionekana kuwa na mantiki na kwa manufaa kibinadamu, Mungu alijua jambo lile lingeufanya ufalme wa Yuda kuwa chini ya utawala wa taifa la kigeni siku zote. 



Madhara yake yalikuwa makubwa mno. Kwa hiyo, Bwana alimtuma Isaya kumwendea mfalme (ambaye inawezekana alikuwa akikagua mfumo wa usambazaji wa maji katika mji wa Yerusalemu kama sehemu ya maandalizi ya kufanya uvamizi) ili kumshawishi asiende kutafuta msaada kutoka kwa kiongozi wa Waashuru. 



Ni kwa nini Bwana alimwagiza Isaya aende na mwanaye, Shear-yashubu (Isa. 7:3)?



Ni hakika kuwa Ahazi alishtuka wakati Isaya alipomtambulisha mwanawe, aliyeitwa “Waliosalia Watarudi.” Waliosalia kutoka miongoni mwa akina nani? Watarudi kutoka wapi? Kwa kuwa baba wa kijana alikuwa nabii, jina lake lilisikika kama ujumbe wa kutisha kutoka kwa Mungu kuhusu wao kutekwa na kupelekwa uhamishoni. Au ulihusu kumrudia Mungu kwa njia ya toba (kitenzi “rudi” kinabeba pia maana ya kutubu)? Ujumbe wa Mungu kwa Ahazi ulikuwa: Maana yake ni vile wewe utakavyochagua iwe! Acha dhambi zako au nenda uhamishoni na kutoka huko uhamishoni waliosalia watarudi. Uamuzi ni wako! 



Ujumbe ulielezeaje hali ya mfalme? Isa. 7:4-9.

Tishio la Shamu na Israeli lingepita na Yuda ingepona. Mamlaka ambazo Ahazi aliziona kuwa kama moto mkubwa wa volkano kwa Mungu zilikuwa tu kama "mikia ... miwili ya vinga ... vitokavyo moshi" (Isa. 7:4). Hakukuwa na haja ya Ahazi kutafuta msaada kutoka Ashuru. 



Lakini ili kufanya uamuzi sahihi, Ahazi alitakiwa kumwamini Bwana na kuziamini ahadi Zake. Alitakiwa kuamini ili kuthibitika (Isa. 7:9). Maneno ya Kiebrania yaliyotafsiriwa “amini” na “thibitika” yana mzizi mmoja wa Kiebrania, ambao ndio pia unaozaa neno “ukweli” (jambo lenye uhakika) na neno Amina (kukubaliana na jambo lililo la kweli/hakika). Ahazi alihitaji kuwa na uthabiti ili kuthibitishwa; alihitaji kutegemea ili kutegemewa. 



Tazama sehemu ya mwisho ya Isaya 7:9. Kwa nini imani na uhakika ni vya muhimu ili “kuthibitika”? Kuthibitishwa katika jambo gani? Ni kwa jinsi gani kanuni hii hutumika katika maisha ya Ukristo?

No comments