amka na Bwana

KESHA LA ASUBUHI

Jumatatu 11/01/2021

*UPATANISHO KWANZA*

*Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako..*Mathayo 5:23, 24*

 *Wakati ambapo wajibu wetu umewekwa wazi, kwa nini washiriki wengi wa kanisa huenda kinyume na “Hivi ndivyo asemavyo Bwana,”* na kuzungumza juu ya magumu yao kwa wale wasiojua chochote kuhusiana nao au kwa habari za wale ambao magumu hayo yanawahusu? Yesu Mwalimu mkuu, ametuambia wajibu wetu. Vipawa vyetu, maombi yetu hayakubaliki kwa Mungu tunapoacha wajibu huu bila kufanywa, na kuruhusu sumu ya husuda, shuku mbaya, na wivu kutawala nafsi zetu, na kuharibu muungano na furaha. Ni kukosa furaha kiasi gani kungeachwa na mawazo maovu kiasi gani yangezimwa ikiwa waumini wangetenda kazi ambayo Kristo amesema ni lazima ifanyike ili kuzuia mawazo maovu na mazungumzo yasiyofaa. 

Maneno machache ya ufafanuzi yanaweza kubadilisha kabisa mawazo ya wale ambao wamekuwa na kutofautiana, wakishikilia hisia chungu. *Hatuwezi kuwa watiifu kwa sheria ya Mungu mpaka tuondoe mawazoni tofauti zote, mpaka turuhusu mioyo yetu ilainishwe na kushindwa na Roho ya Kristo. Maombi yetu yanazuiwa na kiburi cha moyo, kwa kukataa kukiri makosa na kuondoa mivuto mibaya.* 

Tunapaswa kufanya kila jitihada katika uwezo wetu kuondoa kila jiwe la kujikwaa toka mbele ya miguu ya jirani yetu au ndugu yetu. Mwanangu [Edson], fanya kila ridhaa inayowezekana kwako kufanya, usiache katika akili inayoumia uelewa mbaya ambao kutangulia kujishusha na moyo wa upole vingeondoa. Shetani atakuja kwa hakikia katika akili hiyo na jaribu kuleta uelewa mbaya na kujenga mlima katika kichuguu. *Akili inayojikwaa kwa urahisi kutokana na hisia za maumivu itaamsha mawazo yasiyo sahihi ya kila namna*

 *Bwana Yesu ametoa maelekezo ya pekee ya kile ambacho kila "mtoto wake mdogo" anapaswa kufanya. Tunapoomba, "Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu," je, tunafanya sehemu yetu katika kujibu ombi hili?... Ikiwa ndugu yetu ana neno dhidi yetu, tunapaswa kuiacha sadaka tuliyoileta kwa Mungu madhabahuni, na kupatana na ndugu yetu. Kisha turudi kutoa sadaka yetu. Hii ndiyo njia pekee tunayoweza kuhifadhi mioyoni mwetu amani ya Mungu.*

*TAFAKARI NJEMA MUNGU AKUBARIKI SANA MPENDWA*

No comments